• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujenga matumaini mapya ya maisha

    (GMT+08:00) 2010-02-25 12:41:03

    Mwaka mmoja na nusu umepita tangu tetemeko kubwa la ardhi lilipotokea tarehe 12 Mei mkoani Sichuan. Hivi sasa ujenzi wa baadhi ya miradi ya ukarabati wa sehemu zilizokumbwa na tetemeko la ardhi umekamilika, na ujenzi wa miradi mingine unaendelea bila matatizo. Katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, ambayo ni sikukuu kubwa zaidi ya Wachina, watu wa sehemu hizo walisherehekea sikukuu hiyo kwa furaha.

    Bibi Yi Jianping na jamaa zake waliishi katika tarafa ya Yinxiu yenye mandhari nzuri, lakini tarafa hiyo iliharibiwa vibaya kutokana na tetemeko kubwa la ardhi. Nyumba ya bibi Yi Jianping ilibomoka kabisa, lakini kwa bahati nzuri jamaa zake wote walinusurika. Baada ya tetemeko hilo walikuwa wanaishi katika nyumba ya muda, lakini hivi sasa wanaishi katika kijiji cha Yinxing, ambacho si mbali na tarafa ya Yinxiu. Bibi Yi Jianping alisema hivi sasa, tarafa ya Yinxiu inafanya ukarabati, na wanasubiri kuhamishiwa katika nyumba mpya baada ya ujenzi wa nyumba kukamilika. Alisema,

    "Hivi sasa tarafa ya Yinxiu inajenga nyumba mpya, kwa hiyo tunahamia hapa."

    Bibi Yi Jianping alisema nyumba za kijiji cha Yinxing hazikuharibiwa sana, hivyo baada ya kukarabatiwa wanaishi hapo kwa muda. Ujenzi wa nyumba mpya za tarafa ya Yinxiu utakamilika kabla ya tarehe 12 Mei mwaka huu, wakati huo wataweza kuhamia katika nyumba mpya.

    Baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, bibi Yi Jianping anafanya kazi ya usafi katika ofisi za serikali ya tarafa ya Yinxiu, ingawa kazi hiyo ni ya uchovu, lakini anafurahi kila siku kwa kuwa anaweza kujenga maisha yenye furaha kwa mikono yake. Wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, mume wake ambaye anafanya kazi za vibarua katika sehemu nyingine alirudi nyumbani, na watoto wake wanaosoma katika sehemu nyingine pia walipumzika na kurudi nyumbani. Jamaa wote walirudi nyumbani na kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, bibi Yi Jianping alifurahi sana.

    Serikali ya huko iliwapa watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi nguo, chakula na mafuta ya kupikia, lakini bibi Yi Jianping alitaka kununua vitu vingi zaidi. Alisema ingawa sasa ana kazi nyingi, lakini alitaka kununua nguo mpya kwa kila mtu wa familia yake, na kutayarisha chakula kizuri cha mkesha wa mwaka mpya wa jadi, ili waweze kusherehekea pamoja sikukuu hiyo kwa furaha.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako