• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujenga matumaini mapya ya maisha

    (GMT+08:00) 2010-02-25 12:41:03

    Kama alivyo bibi Yi Jianping, Bw. Xian Tianquan aliyekuwa anaishi kwenye kijiji cha Penghua mjini Mianzhu pia alikumbwa na tetemeko la ardhi. Kabla ya tetemeko hilo, Bw. Xian Tianquan alikuwa anajishughulisha na kazi ya kuwapokea watalii nyumbani kwake, ambapo watalii wanaweza kula, kulala na kujiburudisha kwa michezo. Lakini nyumba yake iliharibiwa vibaya kwenye tetemeko la ardhi, na mke wake pia alifariki kutokana na tetemeko hilo. Kwa kuwa serikali ya China ilianza kufanya ukarabati mara baada ya tetemeko, hivyo Bw. Xian Tianquan alihamia kwenye nyumba mpya mwanzoni mwa mwaka 2009. Kutokana na misaada mbalimbali, Bw. Xian Tianquan mwenye umri wa miaka zaidi ya 50 hakufa moyo, bali alikuwa na matarajio mapya kuhusu maisha yake. Alisema,

    "Baada ya nyumba mpya kujengwa mwaka 2009, nilikuwa na familia mpya. Tarehe 8 mwezi wa kwanza wa mwaka 2009 kwa kalenda ya kilimo ya China, biashara yangu ya furaha ya familia za wakulima nayo ilianza tena."

    Bw. Xian Tianquan alisema mwanzoni mwa mwaka 2009, kutokana na msaada aliopata kutoka kwa jamaa na marafiki zao, biashara ya kuwapokea watalii ilianza tena katika nyumba yake mpya. Baadaye alifahamiana na mwanamke mmoja kutoka mji wa Meishan, wakapendana na kuoana mwezi Juni mwaka jana. Alisema ingawa yalitokea maafa makubwa, ambayo yalisababisha hasara kubwa, lakini kuwa na familia mpya ni faraja kwake, na mke wake anamsaidia sana. Alisema kadiri ukarabati baada ya maafa unavyoendelea vizuri, ndivyo watu wa sehemu hizo wanavyohamia kwenye nyumba mpya, ambazo mazingira yake yameboreshwa kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo watu wengi wanaoishi mijini wanakwenda kutalii vijijini, na biashara yake imekuwa nzuri kuliko zamani. Bw. Xian alisema,

    "Kutokana na hali ya hivi sasa, mapato ya mwaka wa kwanza baada ya kuanzishwa upya shughuli za "kuwapokea watalii" yamekuwa makubwa, nina furaha sana."

    Bw. Xian Tianquan alisema mwaka jana alipata Yuan zaidi ya elfu 50 kutokana na shughuli zake, na anaamini kuwa mapato ya mwaka huu yatakuwa mazuri zaidi. Binti yake pia alihitimu kutoka chuo kikuu mwaka jana, sasa amekuwa daktari katika hospitali moja mjini Mianzhu. Bw. Xian Tianquan alisema wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Spring, watalii wengi walikuja kutalii vijijini, wakati huo alikuwa na shughuli nyingi. Hivyo mwanzoni mwa sikukuu hiyo, alianza kufanya maandalizi kwa ajili ya shughuli za sikukuu hiyo. Alisema,

    "Nilitayarisha baadhi ya vitu kwa ajili ya sikukuu ya Spring, kama vile kuku na bata."

    Bw. Xian Tianquan alisema, maisha ya sasa yamekuwa mazuri zaidi kuliko yale ya kabla ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, sio tu nyumba mpya imekuwa imara na kubwa zaidi, bali pia mazingira ya makazi yamekuwa safi zaidi. Bw. Xian Tianquan alisema, hivi sasa maisha yamekuwa mazuri, hivyo atafanya juhudi zaidi ili maisha yake yawe mazuri zaidi mwaka hadi mwaka. Alisema,

    "Watu wote wanafurahi, na jamaa wanajumuika ili kusherehekea sikukuu ya Spring kwa furaha. Matumaini yangu katika mwaka mpya ni kwamba: mwaka jana umepita, na nitajitahidi zaidi katika mwaka mpya, ili kuzifanya vizuri zaidi shughuli za kuwapokea watalii".


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako