• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea jumba la maonesho la Lithuania

    (GMT+08:00) 2010-11-09 15:41:52

    Maputo ya joto, mpira wa kikapu, chakula kitamu na ambariā€¦ maneno hayo yanaonekana kama haya uhusiano wowote kati yao, lakini yanahusiana na Lithuania, nchi iliyoko kwenye pwani ya bahari ya Baltic. Sehemu ya nje inayopendeza ya jumba la Lithuania kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai ilionesha umaalumu wa utamaduni wa nchi hiyo ya kale na kuvutia watazamani wengi.

    Katika karne ya 14 na 15 Lithuania ilikuwa ni nchi ya Ulaya yenye eneo kubwa zaidi, kwa hiyo watalii wanaotembelea jumba hilo wanaweza kufahamishwa mambo mengi sana kuhusu nchi hiyo. Lakini hivi sasa maputo ya joto ni kitu kinachofuatiliwa na watu wengi kuhusu nchi hiyo, hata katika jumba la maonesho ya Lithuania. Mkuu wa jumba la maonesho la Lithuania Bi Indre Kumpikeviciute alisema,

    "Maputo joto yalitiliwa mkazo zaidi katika usanifu wa jumba la Lithuania, kwani mji mkuu wa Lithuania, Vilnius ni kati ya miji mikuu ya nchi chache za Ulaya, ambayo watu wa kawaida wanaruhusiwa kuangalia mandhari ya mji wakiwa kwenye maputo ya joto angani."

    Lithuania ni nchi yenye idadi kubwa ya maputo ya joto kwa wastani wa idadi ya watu, vilevile ni nchi yenye idadi kubwa ya waendeshaji wanawake wa maputo ya joto duniani. Katika mji mkuu Vilnius watu wakitaka kuangalia mandhari ya mji wakiwa katika maputo ya joto angani wanapaswa kulipa Euro 100 kwa saa 1 au kwa saa 2. Lakini watazamaji wanaotembelea jumba la maonesho la Lithuania, wanaweza kuhisi hali ya kuwa angani kwa maputo ya joto bila kulipa pesa, ambapo wanaweza kuona mtaa na ncha ya mnara wa kanisa lenye mtindo wa kipindi cha historia cha ustawi wa uandishi na sanaa. Wasanifu wa jumba la Lithuania walijenga kielelezo cha puto la joto katikati ya jumba la Lithuania, ili watazamaji waweze kuwa karibu nalo. Mkuu wa jumba la maonesho Bi Kumpikeviciute alisema,

    "Katika kielelezo cha puto la joto, watu wanaweza kuhisi hali ya kupaa angani wakiwa katika puto la joto, na kuona sinema inayowafahamisha kuhusu nchi hiyo, hususan wanaweza kusema matarajio yao kwenye jiwe moja lililowekwa kando ya puto la joto."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako