• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea jumba la maonesho la Lithuania

    (GMT+08:00) 2010-11-09 15:41:52

    Mkuu wa jumba la maonesho alisema jiwe hilo la kueleza matarajio ni jiwe la kweli lililotoka kwenye uwanja wa kanisa kubwa la mjji wa Vilnius. Walithuania wengi ni wakatoliki, kwa hiyo jiwe hilo limekuwa ujumbe wa utamaduni wa dini nchini Lithuania.

    Lakini watu wengi zaidi wanaifahamu Lithuania kutokana na mpira wa kikapu. Mafanikio makubwa ya timu ya mpira wa kikapu ya Lithuania na Bw Yunus Kazi Lao Ilgauskas, kocha mashuhuri wa timu ya mpira wa Kikapu ya wanaume kutoka Lithuania wanawafanya watu wengi waifahamu nchi hiyo. Watazamaji wanaweza kucheza pamoja na wafanyakazi wa jumba la Lithuania kwenye uwanja wa mpira wa Kikapu uliojengwa mahususi kwenye upande wa kulia wa jumba la maonesho la nchi hiyo.

    Mwishoni mwa mwezi Agosti, jumba la meonesho la Lithuania liliandaa mchezo wa ubingwa wa mpira wa kikapu wa maonesho ya kimataifa ya Shanghai, nchi zote zilizoshiriki kwenye maonesho ya kimataifa ziliweza kuleta timu zao kushiriki. Hii ilikuwa fursa nzuri ya mawasiliano kati ya nchi mbalimbali washiriki. Kuhusu mchezo huo, mfanyakazi wa jumba la Lithuania alisema,

    "tuliandaa mchezo huo, ninatarajia kuwa timu ya Lithuania itaingia kwenye nafasi 5 za mwanzo."

    Watu waliokosa mchezo wa mpira wa kikapu wa maonesho ya kimataifa yaliyofanyika mwishoni mwa Agosti hawapaswi kusikitika sana, kwani kocha mashuhuri wa mpira wa kikapu wa Lithuania Bw Yunus Kazlauskas alijitokeza tena kwenye jumba la maonesho la nchi hiyo mwishoni mwa Septemba. Mkuu wa jumba la maonesho la Lithuania Bi Kumpikeviciute alidokeza akisema:

    "Yunus ni rafiki mkubwa wa Yao Ming, Yunus alimwalika Yao Ming kutembelea pamoja jumba la maonesho la Lithuania."

    Hivyo, watazamaji waliotembelea jumba la Lithuania licha ya kuwa na fursa ya kumwona kocha Yunas, waliweza pia kumwona Yao Ming kwenye jumba la Lithuania lililoko katika maonesho ya kimataifa ya Shanghai.

    Baada ya kujiburudisha kwenye puto la joto na kucheza mpira wa kikapu, pengine watalii wanaweza kuwa wamechoka kidogo. Mkahawa mmoja wa jadi wa Lithuania ulioko sehemu ya nyuma ya jumba la maonesho la Lithuania ni sehemu nzuri ya kupumzika, huko watu wanaweza kupata chakula halisi kizuri cha nchi hiyo. Bia za Lithuania pia zimeahi kupata tuzo nyingi za kimataifa, ikilinganishwa na bia za nchi nyingine, Bia za Lithuania zina alcohol nyingi, hivyo ni kali kidogo. Kama wewe ni mpenzi wa bia, basi usikubali kuikosa. Mfanyakazi wa kike wa jumba la maonesho la Lithuania Bi Ruta Sakalauskaite aliwafahamisha watu kuhusu maandazi yenye viazi na nyama ndani yake yanayoitwa Cepelinai. Alisema,

    "Hiki ni kitoweo halisi cha Lithuania, umbo lake linafanana na "meli ya angani", nyama, ham iliyofukizwa kwa moshi pamoja na uyoga vinatiwa ndani ya viazi, viazi viko katika umbo lake la zamani, kisha vinapikwa. Jina la kitoweo hicho linatokana na hayo, katika lugha ya Kilithuania, cepelinai ni "meli ya angani".

    Baada ya kufurahishwa katika puto la joto na kuonja chakula kitamu cha Lithuania, mwishoni watalii hawasahau kununua zawadi za kumbukumbu za ambari kwenye jumba la maonesho la Lithuania kwa ajili ya jamaa na marafiki zako. Ni vizuri mkifahamu kuwa 95% ya ambari iko katika kanda ya Leningrad na Lithuania, hivyo ambari ni bidhaa maarufu ya Lithuania. Kabla ya miaka zaidi ya 1,000 iliyopita, walithuania walikuwa na shughuli nyingi za biashara pamoja na Dola la warumi, na kulikuwa na "Njia ya Ambari", ambayo ilikuwa muhimu katika historia ya Lithuania kama "Njia ya Hariri" ya kale ya China.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako