• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jun Yihao, shabiki wa majumba ya makumbusho

    (GMT+08:00) 2011-07-11 19:41:41

    Katika kitongoji kilichoko kaskazini mwa Beijing, kuna nyumba moja yenye bustani. Mwenye nyumba hiyo Bw. Jun Yihao ana umri wa miaka 47 ni msanii, mhifadhi wa vitu vya mabaki ya kale na mfadhili. Zaidi ya hayo yeye pia ni shabiki wa majumba ya makumbusho. Si kama tu Bw Jun anatembelea majumba ya makumbusho katika sehemu mbalimbali duniani, bali pia anajenga majumba maalumu ya makumbusho nchini China kwa ajili ya watoto wanafunzi. Mwandishi wetu wa habari alimtembelea Bw Jun Yihao na jumba lake la makumbusho. ..

    Kinachovutia zaidi macho kwenye bustani ya Bw Jun ni yeye mwenyewe. Alinionesha picha zilizochorwa, vinyago, vielelezo vya dinosaur, na sampuli za mawe na mbao, vitu ambavyo alivikusanya na kuanzisha jumba la makumbusho la aina yake. Toka mwaka 1998 Bw Jun amekuwa akijenga majumba zaidi ya 600 ya namna hii katika shule za msingi na sekondari katika sehemu mbalimbali za China.

    Bw. Jun alisema "Watoto wa shuleni wanapewa matarajio makubwa ya kupata mafanikio katika masomo yao. Hawana fursa wala uwezo wa kutembelea majumba muhimu ya makumbusho kote duniani. Na watoto wanaoishi katika sehemu za vijijini hawana fursa kabisa ya kutembelea majumba la makumbusho. Mimi sina uwezo wa kuwatoa kutoka kwenye ratiba ngumu ya masomo shuleni, kwa hiyo najenga majumba ya makumbusho ndani ya shule kwa ajili ya watoto hao."

    Bw Jun Yihao alizaliwa mwaka 1963 katika familia ya walimu. Maskani yake ni sehemu inayopendeza yenye mito na maziwa mengi, ndiyo maana alivutiwa na usanii tangu alipokuwa mtoto.

    Alisema "Nilipokuwa na umri wa miaka 15, niliona natakiwa kumpata mwalimu atayenifundisha kuchora picha. Kwa hiyo nilimpata msanii maarufu, nilihamia nyumbani kwake na kuwa mpishi wa familia yake. Msanii huyo ana marafiki wengi wasanii, na kila baada ya tafrija za marafiki hao, walianza kuchora picha au kuandika maandishi ya Kichina, walinipa kazi nyingi kama zawadi."

    Huu ndio ni mwanzo wa Bw Jun kukusanya vitu vya sanaa. Baadaye aliondoka maskani yake na kuelekea Beijing na London, ambapo alivutiwa na kazi nzuri za sanaa alizoziona katika majumba makubwa ya makumbusho. Katika matembezi yake alipata wazo moja, naweza kutengeneza nakala za kazi hizo za sanaa na kuzionesha katika sehemu ya vijijini nchini China.

    Katika majumba ya makumbusho yaliyojengwa na Bw Jun, kazi zote za sanaa zinaoneshwa wazi, hakuna chochote kinachowazuia watazamaji kuangalia kwa karibu. Bw Jun alisema

    "Katika majumba ya makumbusho, ni kawaida kwa watazamaji kutosogelea sana vitu vinavyooneshwa, ama vinalindwa na kuna kioo kinachozuia au viwekwa ndani ya sanduku. Watazamaji wanaweza tu kuangalia kwa mbali, na ni mwiko kuvigusa na kuvihisi vitu vinavyooneshwa. Lakini mimi napenda watoto waweze kugundua uzuri wa vitu hivyo, naamini kuwa hawataviharibu makusudi. Vile vile watoto wana mitizamo mipya kabisa kuhusu kazi za sanaa."

    Waziri mkuu wa China Wen Jiabao alipoambiwa kuhusu shughuli anazofanya Bw Jun Yihao, alimshukuru hadharani kutokana na kujenga majumba hayo ya makumbusho. Jambo hili lilimletea Bw Jun fahari kubwa. Bw Jun alisema

    "Kihalisi kila mtoto ni hodari katika mambo ya sanaa. Kabla ya kuanza shule ya msingi, uwezo wao wa ubunifu unakuwa hauna vikwazo. Ukichora duara wao wanaona hili ni jua, mwezi, bakuli, sahani, au kitu chochote. Lakini baada ya kupata masomo shuleni, wanadhani picha hii ni sifuri, ni namba moja tu."

    Mbali na shule, Bw Jun pia anajenga majumba ya makumbusho katika sehemu mbalimbali nchini China. Katika sehemu za vijijini ambazo hazimudu ujenzi wa jumba la makumbusho, Bw Jun alifadhili ujenzi huo. Kwa hiyo ametoa ufadhili wa Yuan milioni 30, sawa na dola za kimarekani milioni 5 katika ujenzi wa majumba ya makumbusho katika sehemu za vijijini.

    "Sina matarajio ya kuwafanya watu wapate ujuzi fulani fulani kutoka katika majumba yangu ya makumbusho. Badala yake wanaweza kupata burudani na hisia kutokana na kazi za sanaa zinazooneshwa. Pia nina imani kuwa kila mmoja anapata anachotaka nje ya majumba ya makumbusho."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako