• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jun Yihao, shabiki wa majumba ya makumbusho

    (GMT+08:00) 2011-07-11 19:41:41
     Jumba la makumbusho la sanaa la taifa lafunguliwa, wananchi wanaweza kuingia bila malipo

    Jumba la makumbusho la sanaa la taifa la China limeanza kuwapokea watazamaji bila kutoza kiingilio, likiitikia wito la serikali wa majumba yote ya makumbusho ya umma kutoa huduma kwa umma bila kutoza kiingilio.

    Awali jumba hilo la makumbusho la sanaa ambalo liko Beijing na linahifadhi kazi zaidi ya laki moja za sanaa, lilikuwa bila kutoza kiingilio kwa watazamaji kwa ajili ya maonesho muhimu na katika sikukuu kubwa. Hadi sasa watu elfu 5 wametembelea jumba hilo toka lianze kuruhusu watu kuingia bila kiingilio. Mtazamaji mmoja alisema

    "Mimi si mkazi wa Beijing, natoka mji wa Guilin. Naona Beijing ina mazingira mazuri sana ya usanii. Kuweza kutembelea na kuangalia kazi za sanaa bila kizuizi chochote ni muhimu sana kwetu sisi watu wa kawaida zaidi kuliko kuokoa pesa kadhaa."

    Mkurugenzi wa jumba la makumbusho la sanaa la China Bw Fan Di'an alieleza mpango wa jumba hilo kuwa, wataingiza vitu vya aina nyingi vya sanaa kwenye jumba hilo, vikiwemo vinavyohusu kazi za sanaa za kisasa. Alisema

    "Kila mwezi mbali na kuandaa maonesho makubwa, pia tutaandaa maonesho madogo na ya kati kwa ajili ya sanaa mpya. Haya ni mageuzi ya maonesho yetu. Watazamaji wataweza kupata sura ya jumla ya maendeleo ya sanaa, na pia watapata mtazamo tofauti kuhusu sanaa."

    Jumba la makumbusho la sanaa la taifa la China linatoa bure tiketi elfu 6 kila siku, na tiketi elfu 2 kati ya hizo zinapatikana baada ya kujiandikisha kwenye tovuti ya jumba hilo. Kuanzia mwaka 2008 China ilianza mchakato wa kufungua majumba ya makumbusho bila malipo, ingawa hadi sasa bado kuna baadhi ya majumba ambayo yanaendelea kuwatoza kiingilio watazamaji.

    Wizara ya utamaduni ya China na wizara ya fedha ya China zilitoa wito kwa pamoja mwezi Februari, kwamba majumba yote ya makumbusho ya umma yanatakiwa kuanza kutoa huduma kwa umma bila malipo ndani ya miaka miwili.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako