• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dereva mmoja wa baiskeli yenye magurudumu matatu mjini Shaoxing

    (GMT+08:00) 2011-07-15 15:00:23

    Ni jumapili asubuhi. Meng Xueqing anaondoka nyumbani saa 2, anaendesha baiskeli yake yenye magurudumu matatu kuelekea mtaa wa makazi ya Lu Xun, ambaye ni mwandishi wa zamani wa vitabu anayejulikana sana nchini China. mtaa huo umekuwa kivutio vha utalii kwa watu. ..

    Meng anasema katika siku za kazi, anasubiri wateja nje ya hospitali na hoteli, lakini wakati wa wikiendi, anapendelea kwenda kusubiri katika maeneo yenye vivutio vya utalii, kwani huko ni rahisi zaidi kupata wateja. Meng ameishi maisha yake yote mjini Shaoxing, na amewahi kufanya kazi katika kiwanda, ambacho kilifilisika miaka kumi iliyopita, ambapo alilazimika kuanza maisha mapya kama dereva wa baiskeli yenye magurudumu matatu. Anasema kuchuma pesa siyo sababu iliyomfanya aamue kuwa dereva wa baiskeli hiyo.

    "sasa nimeanza kuzeeka. Wakati wa majira ya joto huwa natokwa na jasho jingi na wakati wa majira ya baridi nasikia baridi kidogo. Sitarajii kupata pesa nyingi katika kazi hii. Ninafurahi kama nina pesa za kutosha kula. Wakati mwingine naona kutembelea mahali mbalimbali hapa Shaoxing na kuongea watu mbalimbali ni jambo lenye furaha."

    Sasa ni likizo ya majira ya joto, watalii wengi wanamiminika mjini Shaoxing. Dakika tano tu baada ya kufika kwenye mtaa wa makazi ya Lu Xun, mtalii mmoja anamtaka Meng amtembeze katika mji huo. Bw Meng anasema anapenda sana kuwatembeza watalii katika mji wa Shaoxing.

    "Shao Xing ni mji maarufu sana. Kuna sehemu nyingi za vivutio kama vile Daraja la Baozhu na Daraja la Bazi. Pia kuna mitaa mingi ya kale inayovutia ambayo ni yenye historia ndefu kama vile mtaa wa Cang Qiao, ambapo unaweza kuona nyumba zenye umaalumu wa Shaoxing katika zama za kale, ambazo baadhi yao zimekuwa baa za kahawa."

    Wakati anapowatembeza watalii kwenye eneo la vivutio vya utalii, bila ya kujizuia anaonesha mapenzi aliyonayo kwa maskani yake. Mkononi mwake, ana kitabu cha kuwaelekeza wasafiri chenye picha nzuri za vivutio vingi vya utalii mjini Shaoxing. Kwa sasa anaonekana kama mwongozaji watalii kuliko dereva wa baiskeli yenye magurudumu matatu.

    Baada ya zaidi ya nusu saa, Bw Meng anarudi kwenye kituo chake, na kwa kuwa ni siku za majira ya joto, mjini Shaoxing kuna joto sana. Anakunja suruali yake, na shati lake kubwa linakuwa limelowa jasho. Hata hivyo, sura yake bado inakuwa inaonesha tabasamu.

    Bw Meng anasema kuna madereva zaidi ya elfu 5 wa baiskeli zenye magurudumu matatu mjini Shaoxing. Mwaka jana, idara husika za mji huo zilikangaza kanuni kuhusu kila baiskeli ya namna hiyo ipewe namba, kama ilivyo kwa teksi. Nambari zote zinatolewa bure, na madereva wanaweza kununua baiskeli hizo kwa Yuan kati ya 200 na 300, na kisha kwenda katika idara husika kupewa namba.

    "serikali inatuhudumia vyema. Si kama tu inatupa namba, bali pia inatupa sare ya waendesha baiskeli zenye magurudumu matatu, ambayo inatufanya tuwe kama wa kundi moja. Katika miaka ya hivi karibuni, Shaoxing imeshuhudia maendeleo makubwa. Watu wengi wameanza kuufahamu mji huu mdogo, na hii imesaidia kukuza biashara yetu. Mandhari ya mji imezidi kuwa nzuri zaidi kuliko, lakini bado mji unadumisha majengo ya zamani. Maisha yetu yanakuwa mazuri siku hadi siku."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako