• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dereva mmoja wa baiskeli yenye magurudumu matatu mjini Shaoxing

    (GMT+08:00) 2011-07-15 15:00:23
    Jua ni kali sana, na ni wakati wa chakula cha mchana. Bw Meng anafungua mfuko wake na kuchukua boksi la kuhifadhia chakula ambacho kimeandaliwa na mkewe. Bw Meng anasema chakula kinachoandaliwa na mkewe ni kitamu mno duniani.

    "mke wangu anafanya kazi katika shule ya chekechea. Yeye ni mpishi hodari. Watoto na walimu wa shule hiyo wanamsifu sana. Tuna mtoto mmoja wa kiume, ambaye ni hodari sana katika masomo tangu alipokuwa mtoto. Mwaka jana alimwoa mwanafunzi mwenzake wa chuo kikuu. Sasa wanaishi huko Jinhua, mji mwingine mdogo katika mkoa wetu. Ametuambia mara nyingi mimi na mke wangu tuhamie katika mji wao, lakini nimekataa. Nimemwambia wakatapokuwa na mtoto, tutakwenda Jinhua kuwasaidia".

    Anaonesha kufurahia kila anapozungumzia familia yake. Anasema kila siku, anaweza kupata yuan kati ya 30 na 40 kwa wastani, ingawa ni pesa ndogo, lakini hajali sana. Anasema kabla ya kuwa dereva wa baiskeli yenye magurudumu matatu, alikuwa na shinikizo la damu, lakini sasa limetoweka. Alisema kama akikaa nyumbani kila siku basi atanenepa na kuzeeka haraka.

    Joto linaendelea kuongezeka. Baada ya kumaliza chakula hicho, Meng anatumia leso kupangusa jasho na kusubiri tena wateja. Baadhi wa wakati, anaongea na marafiki zake ambao pia ni madereva wa baiskeli zenye magurudumu matatu.

    Kadri mji wa Shaoxing unavyozidi kustawi, ndivyo watu kutoka sehemu mbalimbali wanakwenda Shaoxing kuwa madereva wa baiskeli zenye magurudumu matatu. Bw Meng anasema hana wasiwasi na watu hao, haoni kama kuwa kuja kwao kutakuwa changamoto kwa madereva wa huko.

    "hapana, sidhani kama watachukua biashara yetu. Nafanya kazi hii kwani napenda kuwa mtu anayetembea kila siku na kuongea na watu mbalimbali. Sitarajii kupata pesa nyingi, nataka kuishi maisha ya furaha. Wanakuja hapa kutafuta pesa ili waweze kuishi maisha mazuri zaidi. Hivyo kwanini tusishirikiane nao katika fursa hii?"

    Bw Meng anasema pesa siyo muhimu sana kwake, kitu anachozingatia zaidi ni kuweza kuendesha baiskeli yenye magurudumu matatu ambako kunasaidia kujenga afya yake na kumpa furaha. Anajivunia kuwa anaweza kuwa mwongozaji wa watalii mjini Shaoxing. Anasema kama hali yake itaendelea vizuri, ataendelea kuendesha baiskeli yenye magurudumu matatu.

    Upepo mwanana unavuma na jua linaanza kuzama. Ni saa moja jioni. Bw Meng anasema kila siku wakati kama huu, anarudi nyumbani na kula chakula cha jioni na mkewe.

    Kutokana na jinsi uso wa Meng unavyoonekana, hatuwezi kugundua kama amechoka, na kama ana maumivu kutokana na pilika za maisha ya kila siku. Kwa watu wengi wanaoishi kwenye miji mikubwa nchini China, kuwa na pesa nyingi na kununua nyumba kubwa vinamaanisha furaha maishani. Lakini kwa Bw Meng, dereva wa baiskeli yenye magurudumu matatu ambaye anapata Yuan 900 tu kwa mwezi na kuishi kwenye mji mdogo, maisha mazuri kwake ni kuwa na afya nzuri na familia yenye furaha.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako