• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwimbaji wa Afrika aliyetimiza ndoto yake ya muziki nchini China

    (GMT+08:00) 2011-07-25 19:20:48

    Siku hizi video moja inatazamwa sana kwenye mtandao wa internet nchini China. Kwenye video hiyo, kijana mmoja kutoka Afrika anaimba nyimbo za kichina kwa shauku kubwa. Wiki moja baada ya video hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa Internet, tovuti nyingi kubwa za kichina pia ziliionesha, idadi ya watazamaji wa video hiyo imezidi milioni moja. Je, huyu mwimbaji kijana ni nani? Anatoka nchi gani, na kwa nini anapenda kuimba nyimbo za kichina? Mashambiki wengi wa mtandao wa internet hapa China walivutiwa na kijana huyo anayependa kuimba nyimba za kichina. .

    Kijana huyu kutoka Nigeria anaitwa Asabere George, lakini amejipatia jina la kichina Haodi, yaani kaka mdogo mwema. Hivi karibuni mwandishi wetu wa habari alipata fursa ya kuongea naye.

    Haodi alipozungumzia video yake alisema, hata yeye mwenyewe anashangaa kuona kuwa video hiyo imeweza kuwavutia watazamaji wengi namna hii. Mbali na hayo, ingawa hajui kuandika kichina, taarifa 40 hivi alizotoa kwa maandishi ya kichina Pinyin kwenye microblog yake zimevutia wafuatiaji zaidi ya laki tatu. Haodi alisema, hakujua kuwa angeweza kuwa "maarufu namna hii". Kijana huyo kamwe hakufikiria kuwa angekuwa "nyota maarufu" katika nchi ya nje. Haodi alisema:

    "nilipopigiwa video hii sikutarajia kuwa ingewavutia watazamaji wengi namna hii. Zamani kila nilipotazama waimbaji nyota kwenye televisheni, pia nilifikiria kuwa siku moja mimi mwenyewe ningeimba kwenye jukwaa kubwa, nikishangiliwa na watazamaji."

    Kaka yake ndiye mtu aliyemhimiza Haodi adhamirie kuja China kujaribu kutimiza ndoto yake ya muziki. Haodi alisema, kutokana na kupenda muziki, mwaka 1996 kaka yake Haoge aliacha kazi ya uhandisi wa ndege na kuanza juhudi zake za kuwa mwimbaji. Haoge alikuja nchini China mwaka 2002, na mwaka 2006 alishiriki kwenye mashindano ya uimbaji yaliyoandaliwa na televisheni ya taifa ya China CCTV, na alipata tuzo ya pili kwa mwaka huo, akaanza kujulikana nchini China. Mwanzoni Haodi hakuamini kuwa kaka yake kweli amefanikiwa. Alisema akitabasamu,

    "mwanzoni kaka alipotuambia amekuwa mtu anayejulikana nchini China, marafiki zake na ndugu zake huko nyumbani Nigeria sote hatukuamini, tulidhani anatania tu. Tulianza kumwamini pale alipotuonyesha video ambayo alishiriki kwenye maonesho nchini China."

    Hali ambayo maelfu ya watazamaji walimwita kwa sauti kubwa jina la kaka Haoge ilichochea shauku kubwa moyoni mwa Haodi, pia akapata msukumo wa kuja China kujaribu kutimiza ndoto yake. Baada ya kuimba kwa muda katika baa za Beijing, mwaka 2008 Haodi alijiunga bendi ya Wuzhouchangxiang iliyoanzishwa na mwanamuziki wa China Bw. Yu Xin. Waimbaji 6 wa bendi hiyo wanatoka mabara tofauti, lakini wanaweza kushirikiana na kuelewana kutokana na upendo wao kwa muziki.

    Haodi alisema, alipokuwa nyumbani Nigeria, alijifunza kidogo historia ya China, alitazama filamu zilizoigizwa na wanafilamu wa China Jackie Chen na Bruce Lee, pia anafahamu baadhi ya mila na desturi za China. Lakini mwanzoni alipokuja China, Haodi pia alisumbuliwa na tofauti za utamaduni. Alitoa mfano mmoja akisema:

    "nyumbani Nigeria, tukitaka kumpatia mtu kitu, tunatumia mkono wa kulia, lakini hapa China ni tofauti. Siku moja Yu Xin aliponipatia kitu kwa mkono wa kushoto, nilikasirika kidogo nikamwuliza 'kwa nini unatumia mkono wa kushoto', Yu Xin akanijibu kuwa kwa sababu uko hapa China."

    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako