• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwimbaji wa Afrika aliyetimiza ndoto yake ya muziki nchini China

    (GMT+08:00) 2011-07-25 19:20:48

    Yu Xin kamwe hawachukulii waimbaji wa bendi hiyo kuwa ni wageni kutoka nje. Alisema kila watu wawili wana tofauti zao, bila kujali ni wageni au wachina. Jambo muhimu ni kuelewana na kuungana mkono.

    Lakini baadhi ya wakati Haodi huwa anapenda Yu Xin amchukulie kuwa ni mgeni, hasa wakati Yu Xin anapomtaka ajifunze nyimbo ngumu za kichina. Ingawa Haodi anaweza kuongea kichina bila matatizo makubwa, lakini maandishi rasmi kama vile maneno ya nyimbo bado ni m magumu kwake. Haodi alisema siku moja Yu Xin alimwambia ajifunze wimbo mmoja mpya wa kichina, kama kawaida Haodi akakubali. Lakini aliposikiliza rekodi ya wimbo huo, aligundua kuwa hafahamu hata neno moja! Kwa sababu wimbo huo ni sehemu moja maarufu ya opera ya Beijing ,Zhameian. Haodi alisema akicheka:

    "inaonakana kuwa anasahau mimi ni mgeni, nilimpigia simu mara moja, lakini simu yake ilikuwa imezimwa. Kwa hiyo nililazimika kujifunza wimbo huo, lakini siku mbili baada ya klujifunza nilishindwa kukumbuka maneno yake. Baadaye Yu Xin aliniambia kuwa kila mwimbaji wa bendi hiyo ana wimbo wake maalumu, na huo ni wimbo wako, ni lazima ujifunze kuimba vizuri."

    Baada ya kufanya mazoezi kwa bidii, Haodi ameweza kuimba vizuri wimbo huo ambao ni vigumu hata kwa wachina, anajivunia mafanikio yake na akiimba wimbo huo kwa furaha.

    Siku hizi Haodi na bendi ya Wuzhouchangxiang inapendwa na watazamaji wengi wa China kutokana na shauku yao kwa muziki na umaalumu wa kimataifa wa watyu wa bendi hiyo. Katika wimbo wa Changxiangwuzhou waliotunga wenyewe kwa ajili ya michezo ya Olimpiki ya Beijing 2008, sauti ya ngoma ilizopigwa na Haodi iliwafurahisha sana wasikilizaji kutokana na mtindo wake wa kiafrika.

    Haodi alisema, hakutarajia kuwa siku moja anaweza kujiendeleza hapa China, lakini sasa amependa sana nchi hiyo na kutaka kuishi nchini China. Haodi ana ndugu sita wa damu, na yeye ni mtoto wa nne katika familia yake. Sasa kaka yake wa tatu pia ameamua kufuata nyayo za Haoge na Haodi na kuja China kujaribu kutimiza ndoto yake ya muziki.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako