• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Liang Zi kutoka china alitaka zaidi kufahamu utamaduni na desturi za Afrika

    (GMT+08:00) 2014-11-04 17:08:18

    Nchini Eritrea. Mbeleni Liang Zi alikuwa mwanajeshi lakini akajiuzulu kazi yake ili kutembelea nchi mbali mbali za afrika

    "Unajua mwanzoni nilidhania watu barani Afrika wanaishi uchi-yaani bila nguo na pia watu wengi waliniambia watu wengi wa afrika ni wabaya hata wanaweza kunivamia na kunipiga, na pia wengi wao wana magonjwa mengi. Lakini nikasema nataka kujionea ukweli wa mambo kuhusu Afrika. Nikaenda kwenye kijiji kimoja nchini Lesotho kusini mwa Afrika-watu walinikaribisha kwa tabasamu, ni wakarimu sana na hakuna aliyetaka kunidhuru"

    "Kuna mambo mengi muziki, kucheza ngoma…piwa watu wa huko vijijini ni wenye bidii wanajifanyia kila kitu shambani—walinichukua kama mmoja wao tulipika na kula pamoja chakula chao cha kitamaduni na nilikipenda sana..kuanzia wakati huo sikuweza tena kujizuia kwena afrika naenda nchi moja baada ya nyine na nimeandika vitabu sita sasa kuhusu nchi ninazoenda kama vile leshotho, sierra leon Eritrea"

    "Kwenye kila kijiji ninachoienda natafuta mtu mmoja mwenyeji wa kunielekeza na nanunua baiskeli mbili moja yake na yangu….kwa mfano Sierra Leon nimeenda kwenye zaidi ya vijiji 20 na nimehudhuria mazishi, harusi na sherehe ya kuzaliwa mtoto"

    "Wachina wengi bado hawajailewa Afrika na wanafikiria Afrika ni nchi moja, lakini kwenye vitabu vyangu nimewaeleza kwamba Afrika ina nchi 54 na pia utamaduni wa watu, lugha, chakula, mavazi ni tofauti"

    "Naishi kwenye vijiji kwa muda mrefu sio siku 10 ama 20 tu…na ni kwa sababu nataka kujifunza zaidi kutoka kwa wenyeji, kufahamu lugha yao utamaduni vile wanavyoishi, sitaki kuambiwa wala kusoma kwa vitabu lakini nijionee mwenyewe maisha halisi na kuona tofauti kwa mfano ya wakroto na waislamu"

    "Nchini Eretrea wanazungumza lugha ta tigirinya…..lakini nilipenda kukaa na wao tu hata kama sijui lugha walinifunza junsi ya kutengeneza kahawa iliochanganywa na ginger ambayo imekaushwa …wanatengeneza kwa njia ya kitamaduni na ni zuri sana—tunakaa nao usiku na mchana …mmi pia nawafunza kichina na wanaweza kusema maneno ya china…"

    "Kwa jumla nimekuwa nikienda afrika kwa zaidi ya miaka 14 ….mara ya kwanza nilipoenda Afrika sikumwambia mama yangu lakini niliporejea kutoka Lesotho nikaitwa kufanyiwa mahojiano kwenye runinga ---lakini kabla ya mahojiano hayo kurushwa hewani nikaambia mama yangu…nilienda Afrika –akaniuliza…Afrika nchi gani ----nikamwambia Leshotho ….akaniuliza Lesotho ni nini? Kweli alikuwa hajui na watu wengi hawakujua Lesotho hata kwenye mahojiano na vyombo vya habari mara kwa mara walisema Liang Zi amerejea kutoka Soleto"

    "Napenda snaa nchi za Afrika sasa nina marafiki wengi huko….na mimi sitaki kuangalia rangi nyeusi ya ngozi yao kwa sababu kwangu mimi haina maana …sisi wachina tuna ngozi ya majano, wazungu wana ngozi nyeupe lakini sisi wote tuko sawa katika mioyo yetu hatuna tofauti –upendo, familia zinafanana tu…sisi wote tunakula chakula, kupumua hewa moja na kuvaa nguo hivyo tuko sawa"

    "Ninazo kumbukmbu nyingi kwa kila nchi nilioenda afrika..lakini moja ambayo siwezi kusahau ni ya kijiji kimoja nchini Eritrea nilikaa mwezi mmoja na hawakuniruhusu kupiga hata picha moja kwa sababu ni kinyume na dini yao ya kiislam----na wakati huo jamii nilioishi nayo mara walikuwa na maumivu ya kichwa na kwa bahati zuri nilikuwa na dawa za kichina ambazo niliwapa na wakapona…. siku moja chifu wa kijiji hicho na wake zake pia waliumwa na maumivu ya kichwa lakini dawa zilikuwa zimeisha ….nikafikria vile nitawafanya…..nikawafanyia masaji wakapata nafuu….ahh..chifu alifurahi sana akaniambia sasa unaweza kupga picha"


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako