• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Binti Mtanzania nchini China

    (GMT+08:00) 2017-01-06 12:47:41

    Katika mgahawa mmoja ulioko karibu na chuo kikuu cha udaktari cha Tongji, msichana mmoja mwenye macho makubwa kutoka Afrika alipitia menyu kwa haraka akichagua chakula cha mchana na kuagiza kwa kichina. Msichana huyu ambaye anaweza kuongea kichina vizuri ni Mtanzania anayeitwa Anna Mahecha. Mwaka huo utakuwa wa kumi kwake kukaa hapa China.

    Katika mwaka 2006, Anna aliyekuwa akimalizia masomo yake ya sekondari alifanikiwa kupata faraja kutoka serikali ya China kwa kudhaminiwa na kuja China kusoma katika chuo kikuu cha udaktari cha Tongji mjini Wuhan na pia amekuwa msichana pekee kati ya wanafunzi Watanzania 26 waliokuja nchini China mwaka ule.

    "Mimi nilikuwa na furaha lakini pia nilikuwa na hofu, kwa sababu China ni mbali. Baba alifurahi kwani alitaka mtoto wake aishi katika nchi za nje ili ajue mambo mengi. Lakini unajua ile hofu ya mama kwa mtoto wake wa kike, ambaye akimaliza tu kidato cha sita akakwenda mbali mno. Lakini mimi ninafikiri kwamba kuna watu wengi walitaka nafasi hiyo lakini wakakosa, na mimi siwezi kuchezea hii nafasi, niende. Na mwishoni, mama yangu pia aliipokea hali hiyo kwa furaha akaniambia niende tu nikasome kwa bidii."

    Mwaka huohuo, akiwa amebeba ndoto yake na matarajio ya familia, Anna alifika hapa China na kuanza safari yake ya kujifunza. Alipofika kwa mara ya kwanza, alikumbwa na matatizo mbalimbali katika lugha, tabia ya chakula, masomo n.k, lakini wanafunzi wenzake na walimu walimsaidia katika kipindi hicho kigumu.

    "Ningetaka kushuruku wanafunzi wenzangu kwa dhati. Walinichukua kama dada yao na tulikaa vizuri sana.Tulikuwa na umoja na tulifanya mambo mengi pamoja. Na pia wanafunzi wengine na walimu pia walinisaidia Kwa hivyo ingawa nilikumbuka nyumbani sikujisikia upweke. Licha ya lugha ya kichina kuwa ni ngumu, ilichukua muda kujifunza na kuzoea, hakuna tatizo lolote katika maisha ya kawaida."

    Baada ya miaka kadhaa, siyo maisha tu bali hata lugha pia haikumletea tena matatizo Anna. Na sasa Anna amekuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa shahada ya pili katika idara ya udaktari wa magonjwa ya wanawake. Kama wanafunzi wengine wanaosomea udaktari, katika mwaka wa mwisho wa masomo yake, anabeba majukumu mengi zaidi. Licha ya kumaliza utafiti wake, pia anafanya mazoezi ya kazi katika hospitali ya Xiehe ya chuoni kwake.

    Saa moja asubuhi ya mwezi Novemba mjini Wuhan, theluji ilianza kudondoka. Anna alibeba begi kubwa na kutoka. Asubuhi, kama kawaida, anakwenda hospitalini kupiga raundi huku akifuatana na mwalimu wake. Anatembea upesi sana, hata mwandishi wetu hawezi kwenda naye sambamba, alicheka na kusema kuwa tabia hiyo ya kutembea haraka alijifunza kwa wachina.

    Baada ya dakika ishirini, alifika kwenye wodi za magonjwa ya wanawake, akabadilisha nguo na kuanza kazi ya kupiga raundi na kuendelea kupata uzoefu kutoka kwa walimu wake.

    Wakipiga raundi, mwalimu akaeleza mambo mengi juu ya dalili ya magonjwa, na Anna hakuweka kalamu chini, alikuwa akiandika muda wote kwenye daftari ili asikose kitu chochote.

    Mwalimu wa Anna ni hodari sana kwa kushughulikia magonjwa ya saratani ya wanawake, kwa hivyo wagonjwa wake wengi wanasumbuliwa na saratani.

    "kwa mtu wa kawaida akiingia wodini na kuona wagonjwa wengi wenye saratani wanajisikia vibaya sana. Kweli, sote tunajua saratani siyo ugonjwa rahisi kutibika, wagonjwa wanachohitaji kutoka kwetu sisi madaktari siyo huruma tu, bali pia kuwapa matumaini, kwa sababu hawajui wafanye nini na wakikata tamaa kutafanya waumwe zaidi, kwa hivyo madaktari huwa tunawafahamisha ugonjwa wao umefika katika hatua gani na matibabu gani yanayohitajika na kuwasaidia kukabliana na ugonjwa. Watu wanasema madaktari wana roho ngumu, lakini mara nyingi, bora tungesema ni moyo wa ujasiri, dhabiti na pia wenye huruma."

    Baada ya kumaliza kupiga raundi, Anna alichukua begi lake na kwenda kwenye maabara moja kwa moja bila ya kupumzika, kwani bado ana kazi ya kufanywa katika maabara.

    Kuwasha alcohol burner, kusafisha vifaa na kuchukua sampuli, Anna anafanya kazi hatua kwa hatua na kwa umakini mkubwa. Kazi ya maabara ni moja kati ya sekta anazozipenda Anna. Kwa kufanya uchunguzi, anaweza kufanya kazi kwa masaa kadhaa mfululizo.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako