• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Binti Mtanzania nchini China

    (GMT+08:00) 2017-01-06 12:47:41

    Mwalimu wa Anna, mkurugenzi wa idara ya magonjwa ya wanawake wa hospitali ya Xiehe Pro.Wang Hongbo aliwahi kuwafundisha wanafunzi wengi wageni, na alitoa tathmini yake kwa Anna:

    "Yeye anafanya kazi kwa bidii sana, hata kuliko wanafunzi wachina, anasikiliza kwa makini sana darasani na pia anaweza kuuliza maswali baada ya majadiliano.Na anaweza kuongea na wanafunzi wenzake na wagonjwa kwa kichina vizuri. Pia yeye ni mwepesi sana, siku kadhaa zilizopita,alinionyesha uchunguzi mmoja alioufanya, nina shauku kubwa kwani yeye anatumia vizuri sana alichojifunza kwenye uchunguzi huo. Najivunia sana kwa juhudi zake."

    Kujifunza kozi ya udaktari kuna changamoto na shinikizo nyingi, lakini Anna hakuwahi kujuta hata kidogo. Kwani ana sababu nyingi za kuchagua kozi hiyo.

    "Kwanza kozi hiyo kuhusu magonjwa ya kinamama ni kozi muhimu sana. Duniani wanawake ni wengi, kwa mfano, kuna wajawazito wengi, na wakienda kuzaa, wanahitaji watu wa kuwasaidia na pia wagonjwa wako katika sehemu mbali ambapo hakuna madkatari wa kutosha, kama kunawa na watu wengi zaidi wanaojifunza udaktari na kuwa madaktari, basi kutakuwa na madaktari wa kutosha wa kupelekwa katika zile sehemu za mbali kuwasaidia wagonjwa. Na mimi mwenyewe napenda kufanya uchunguzi. Ninapenda kujua vyanzo vyingi vya saratani na namna ya kuzitibu. Pia nataka kutoa mchango yangu pamoja na madaktari wengine nyumbani katika mambo ya udaktari nchini kwangu."

    Miaka ya hivi karibuni, wanafunzi waafrika wengi kama Anna wamekuja hapa China kusoma. China na Afrika zimeshirikiana katika miradi mbalimbali ya sekta ya elimu. Serikali ya China inatoa udhamini kwa wanafunzi Waafirka na kuwahamasisha kuja hapa China kujifunza. Uchunguzi uliofanywa na chombo cha mitandao ya Internet ya Elimu ya China na Kujifunza nchini China umeonyesha kuwa, kuanzia mwaka 2005 hadi 2014, idadi ya wananafunzi Waafrika nchini China inaongezeka kwa kasi kubwa, na kwa wastani ni kwa asilimia 34.69 kila mwaka. Pia takwimu iliyotolewa na wizara ya elimu ya China imeonyesha kuwa mwaka 2015, idadi ya wanafunzi kutoka Afrika imechukua asilimia 12.52 kati ya jumla. Hali hakadhalika, ushirkiano kati ya China na Afrika katika elimu ya udaktari pia unaendelea kwa kasi. Walimu wa ofisi ya kushughulikia mambo ya wanafunzi wageni wa Chuo Kikuu cha Udaktari cha Tongji walisema wanafunzi wao wengi kutoka Afrika wanadhaminiwa na serikali ya China katika ada za shule na matumizi ya maisha. Kwa hivyo, katika mazingira hayo mazuri ya kujifunza, vijana wengi waafrika wanabeba ndoto zao na kuja kusoma hapa China

    Kuna sehemu moja ya kuuza mshikaki karibu na chuo cha Anna, wakati wa usiku ambapo hakuna masomo, Anna hwenda hapo pamoja na marafiki zake wanakaa kidogo na kupiga soga.Yale yaliyomsumbua katika masomo au maisha yote yanaweza kusahaulika mara moja. Vijana hao walioko nchi ya kigeni wanapata furaha na huzuni kwa pamoja na kufanya kila wanavyoweza kutimiza ndoto zao.

    Maisha ya takriban miaka kumi nchini China yanampa hisia kubwa. Anna, anasema kweli ameshajifunza mengi, siyo katika masomo tu, bali pia mawazo na tabia.

    "Kwanza nitoe mfano katika masomo. Wakati nilipoanza masomo ya maabara, nilikuwa sijui chochote cha kufanya, lakini wanafunzi wenzangu wachina walinisaidia kwa moyo wa dhati, hawajali kupoteza muda wao binafsi kunisaidia kadiri wanavyoweza. Nikiwashukuru wanasema hii ni zamu yao ya kunisaidia, kwani wakati walipokuwa hawajui ujuzi huo, watu wengine pia waliwasaidia kwa dhati na wanataka na mimi pia niweze kuwasaidia wengine wanaohitaji msaada, nafikiri kupeana ujuzi huo kweli ni kitendo kizuri sana. Na katika maisha, nimeona Wachina wengi wanajua namna ya kuokoa muda na pesa, nadhani kweli ni tabia nzuri.

    Na katika miaka hiyo karibu kumi, mimi nilisafari mara kwa mara, nimeshakwenda mjini Beijing, Guangzhou, Nanjing n.k, nimeshajionea utamaduni na mandhari tofauti katika sehemu mbalimbali ya China na kweli inafungua macho yangu."

    Baada ya kazi ya siku nzima,hatimaye Anna alirudi bwenini. Alichoka kidogo, lakini hakupumzika hapohapo, bali aliwapigia simu familia yake .

    Tanzania na Beijing zinatofautiana kwa masaa matano, Anna anauliza hali ya nyumbani kwenye simu na kutaka kuisaidia familia yake pale wanapohitaji msaada. Msichana aliyekuwa akilia wakati akikumbwa na matatizo sasa amekuwa thabiti zaidi.

    Wanafunzi wengi wakisoma katika nchi za nje, baada ya kuhitimu huamua kubaki hapohapo kutokana na mazingira mazuri ya kazi na mshahara mzuri. Lakini Anna alisema ana hakika atarudi nyumbani baada ya kumaliza masomo, lakini siyo sasa.

    "Baada ya kuhitimu, ninataka kurudi nyumbani, lakini pia nina tamani kuendelea na masomo, kwa sababu nataka kuwa mwalimu baada ya kurudi nyumbani, kwani nahitaji nifikie katika ngazi fulani. Kwa hivyo nitajitahidi kupata nafasi ya kusoma Phd. Sababu yangu ya kutaka kuwa mwalimu ni kuwa nataka kuwapa ujuzi wangu watu wengine na kufundisha kutafanya watu wengi zaidi kuwa madaktari. Kwa njia hiyo,nitaweza kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi."

    Baada ya kuishi hapa China kwa muda mrefu, Anna hajisikii ugeni tena. Ardhi hii ambayo imeshuhudia furaha na majonzi yake ni kama "nyumba kwao kwa pili". Anataka waafrika wengi zaidi kuja nchini China kujionea maisha ya hapa kama yeye alivyopitia.

    "Na pia napenda kupendekeza waafrika ukipata nafasi ya kuja hapa China kufanya biashara au kusoma au nini, tumia nafasi hiyo vizuri ya kujifunza. Njoo hapa China ujionee mwenyewe utamaduni wake au maisha ya Wachina na usikisie kisie tu kutokana na yaliyosemwa katika televisheni au maneno ya watu wengine."


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako