• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (3 Juni-9 Juni)

    (GMT+08:00) 2017-06-09 19:13:25

    Watu 43 wafariki katika ajali Zimbabwe

    Watu 43 wamepoteza maisha nchini Zimbabwe baada ya basi la abiria walilokuwa wanasafiria kukosa mwelekeo na kugonga mti.

    Msemaji wa Polisi Charity Charamba amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Nyamakate karibu na nchi ya Zambia siku ya Alhamisi.

    Wafanyibiashara mara nyingi hutumia usafiri wa mabasi kati ya nchi hizo mbili kusafirisha bidhaa na kufanya safari nyingine.

    Mwaka uliopita, watu 30 walipoteza maisha wakati abiria waliokuwa wanasafiri kutoka Jijini Harare na Bulawayo kupata ajali.

    Watalaam wanasema kuwa ajali nyingi zimeongezeka katika nchi ya Zimbabwe na nchi zingine za Kusini mwa Afrika kutokana na ubovu wa barabara.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako