• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (1 Juni-7 Juni)

  (GMT+08:00) 2017-07-10 10:43:20
  Jeshi la Niger laua raia 14 kimakosa

  Raia 14 waliuawa siku ya Jumatano Julai 5 na askari wa Niger kijijini kwenye mpaka kati ya Niger na Nigeria karibu na Ziwa Chad, eneo muhimu ambapo kundi la Boko Haram linaendesha harakati zake.

  Wahanga, ambao wote ni wakimbizi, walishukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Boko Haram

  Kwa mujibu wa katibu mkuu wa serikali ya mkoa wa Diffa, Yahaya Godi, miongoni mwa waliouawa kumi na mbili ni raia wa Ngeria na wawili raia wa Niger.

  Watu hao kumi na wanne, walikua wakitoka kupanda pilipili kwenye pembezoni mwa mto Komadougou, kwenye mpaka kati ya Niger na Nigeria katika eneo hilo ambako kunapatikana kijiji kidogo cha Abadam, ambako polisi ya wilaya ya Bosso imekua ikipiga doria.

  Yahaya Godi alisema kuwa Abadam ni kijiji kilichopo katika eneo hatari na limetengwa kwa muda mrefu na kwamba mtu yeyote anayepatikana katika eneo hilo hutambulika kuwa mwanachama wa Boko Haram.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama, viongozi wa mkoa wa Diffa walipata taarifa kama kundi la Boko Haram liko katika kijiji cha Abadam nchini Niger, kwenye mpaka kati ya Niger na Nigeria.

  Jimbo la Diffa limekumbwa na misururu ya mashambulizi yanayotekelezwa na Boko Haram katika miaka ya hivi karibuni.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako