• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (29 Julai-4 Agosti)

    (GMT+08:00) 2017-08-04 20:16:50

    Uganda yaomboleza vifo vya walinzi wake wa amani waliouawa Somalia

    Maofisa wa wizara ya ulinzi wa Uganda na familia za wahanga wamepokea miili ya walinzi 12 wa amani wa nchi hiyo waliouawa na wapiganaji wa Al-Shabaab wakiwa kwenye doria nchini Somalia. Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema vifo hivyo havitabadili dhamira yao ya kutokomeza kundi la Al-Shabaab. Hivi sasa askari 6,500 kutoka Uganda wanashiriki kwenye Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia na kutekeleza majukumu ya kulinda amani.

    Na kwenye shambulizi lingine askari polisi mmoja ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kuvamia kambi ya polisi katika kaunti ya Mandera iliyo mpakani na Somalia.

    Polisi katika kaunti hiyo wamesema, karibu wapiganaji 50 waliokuwa na silaha nzito pia walichoma moto magari mawili na kutoroka na gari moja la polisi.

    Mratibu wa kanda ya Kaskazini mashariki Mohamed Saleh amethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo, na kusema idadi kubwa ya washambuliaji waliuawa wakati wengine kutoroka.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako