• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Septemba-8 Septemba)

  (GMT+08:00) 2017-09-08 21:03:28

  Mwanasiasa wa upinzani Tanzania Tundu Lissu apigwa risasi

  Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amepigwa risasi Alhamisi na watu wasiojulikana mjini Dodoma.

  Kwa mujibu wa taarifa ya chama kikuu cha upinzani CHADEMA kwa vyombo vya habari, tukio hilo lilitokea wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki akiwa nyumbani kwake.

  Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema mbunge huyo ambaye ni mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini

  Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge leo Ijumaa, Ndugai amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye mkono.

  Amesema watu wasiofahamika wakiwa kwenye gari aina ya Nissan ambalo halijajulikana walimpiga risasi kisha kutoweka.

  Hivi karibuni, mbunge huyo kutoka chama cha upinzani cha CHADEMA, amekuwa akikamatwa mara kwa mara na polisi akishutumiwa kufanya uchochezi.

  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako