• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Septemba-8 Septemba)

  (GMT+08:00) 2017-09-08 21:03:28

  Amnesty International yasema Boko Haram yaua watu 400 tangu mwezi Aprili

  Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International linasema kuwa kundi la Boko Haram limewauwa watu 400 tangu mwezi Aprili mwaka huu.

  Amnesty International inasema mauaji mengi yametekelezwa nchini Nigeria na Cameroon, na idadi hii ni mara mbili ikilinganishwa na miezi mitano iliyopita.

  Ripoti ya Shirika hilo inaeleza kuwa, wasichana wadogo walitumiwa na kundi hilo kutekeleza mauaji hayo kwa kujilipua baada ya kufungwa mabomu mwilini.

  Mauaji haya yameelezwa na Amnesty International kama ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na vita vya uhalifu.

  Tangu kuanza kutekeleza mashambulizi mwaka 2009, raia watu 20,000 wameuawa nchini Nigeria na nchi jirani huku wengine Milioni 2.6 wakiyakimbia makwao.

  Amnesty International inataka Jumuiya ya Kimataifa kufanya zaidi kushinda kundi hili.


  1  2  3  4  5  6  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako