• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (9 Septemba-15 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-15 17:46:36

    IGAD yachukua hatua kukabiliana na hali ya wakimbizi nchini Somalia

    Nchi wanachama wa Shirika la maendeleo la kiserikali ya nchi za Afrika Mashariki IGAD wiki hii zimejadili ufumbuzi wa masuala ya mazingira ya wakimbizi na kuwarudisha kwenye jamii wakimbizi wanaorudi nchini Somalia.

    Wajumbe wa IGAD wanaoshughulikia mipango, serikali za mitaa na mambo ya nje walikutana mjini Addis Ababa kujadili hali ya utekelezaji na matokeo ya Mpango wa utekelezaji wa Nairobi, ambao ulitolewa Machi 25 katika Mkutano maalum kuhusu wakimbizi wa Somalia mjini Nairobi. Lengo la mkutano huo ni kukamilisha kazi ya maandalizi ya kuweka mpango wa utekelezaji kuhusu jinsi ya kutekeleza ahadi zilizotolewa na viongozi wa nchi za IGAD na serikali za nchi mbalimbali.

    IGAD pia imesema itatangaza ripoti ya kwanza kuhusu maendeleo ya kazi ya maandalizi ambayo itatathmini maendeleo yaliyopatikana kwa nchi mbalimbali katika Mkutano wa Kikanda wa Kamati ya mawaziri utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako