• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Septemba-29 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-29 18:24:49

    Wapiganaji 13 wa kundi la IS wauawa mashariki mwa Afghanistan

    Wapiganaji 13 wa kundi la IS, akiwemo kiongozi wao mmoja, wameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na jeshi la Afghanistan katika mkoa wa Nangarhar, ulioko mashariki mwa nchi hiyo.

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema, tukio hilo limetokea jana jioni wakati vikosi vya usalama viliposhambulia kwa mabomu maficho ya wapiganaji wa kundi hilo katika eneo la Mohmand Dara wilaya ya Achin.

    Kundi hilo halijatoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.

    Mapema wiki hii, wapiganaji wanne wa kundi la Taliban waliuawa na mwingine kujeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Afghanistan katika wilaya hiyo.

    Na kwingineko huko Afghanistan Waziri wa Ulinzi wa Marekani Bw. James Mattis na katibu mkuu wa NATO Bw. Jens Stoltenberg wiki hii walifanya ziara ya ghafla nchini humo, ikiwa ni mara ya kwanza kwa waziri wa ulinzi wa Marekani kuitembelea nchi hiyo tangu rais Donald Trump atangaze mkakati mpya wa vita katika nchi hiyo mwezi Agosti.

    Bw. Mattis amesema, hadi sasa idadi halisi ya ongezeko la askari wa jeshi la Marekani nchini Afghanistan bado haijajulikana, lakini Marekani itaendelea kuimarisha kikosi cha usalama cha Afghanistan.

    Bw. Stoltenberg amesema, NATO italipatia jeshi la Afghanistan msaada wa dola za kimarekani bilioni 1 kila mwaka hadi mwaka 2020, ili kuisaidia Afghanistan kupambana na ugaidi wa kimataifa.

    Rais Mohammad Asharaf Ghani wa Afghanistan pia ameonesha matumaini yake kwa NATO kuongeza askari nchini Afghanistan kama ilivyofanya Marekani.

    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako