• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (25 Septemba-29 Septemba)

    (GMT+08:00) 2017-09-29 18:24:49

    Hali ya utulivu yarejea mjini Uvira, DRC

    Hali ya utulivu imeanza kureea katika mji wa Uvira, mkoani Kivu Kaskazini, mashariki mwa DR Congo, baada ya waasi wa kundi la Mai mai la CNPSC la William Yakutumba kujaribu kuuteka mji huo.

    Jeshi la FARDC limefaulu kuwatimua wapiganaji wa Mai Mai wanaoongozwa na Wiliam Amuri, almaarufu Yakutumba katika milima ya Uvira, kilomita 20 na mji mkuu wa Burundi, Bujumbura. Wakazi wa mji wa Uvira walisalia ndani, hukua maduka na shule zikifungwa. Shughuli nyingi zilizorota.

    Mpaka wa Burundi na DR Congo ulikua umefungwa kufuatia mapigano hayo. Raia wa Burundi wanaoishi katika maeneo jirani ya Uvira wanasema walipatwa na hofu kubwa baada ya kusikia zana nzito nzito za kijeshi zikirindima tangu asubuhi hadi alaasiri. Inaripotiwa kuwa kuwa askari wa FARDC na wapiganaji ambao walipoteza maisha katika mapigano hayo, upande wa raia haijajulikana.

    Mashahidi wanasema kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) walishiki katika mapigano hayo ambapo ndege zao zilituka kwa kuwashambulia waasi.

    Hata hivyo madai hayo yalikanushwa na Monusco ambayo inasema iliwatuma askari wake katika mitaa ya Uvira ili kuwalinza wananchi, wakimbizi wa ndani na wakimbizi kutoka Burundi, wasiwezi kulengwa katika mashambulizi hayo. Mashahidi wanasema kundi la CNPSC tayari limedhibiti baadhi ya maeneo jirani ya Uvira.

    Mpaka sasa serikali ya DRC inasema watu hao ni majambazi wenye lengo la kuwaibia wananchi, wala hawana nguvu yoyote ya kuudhibiti mji wa Uvira. Wiliam Yakutumba anasema lengo lao ni kumng'oa mamlakani Rais Joseph Kabila.

    Kwa mujibu wa na wakazi wa maeneo jirani upande wa Burundi, askari wengi wa Burundi wametumwa kwenye mpaka na DRC tangu Alhamisi jioni Septmba 28.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako