• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (8 Oktoba-13 Oktoba)

    (GMT+08:00) 2017-10-13 18:55:22

    Serikali ya Kenya yapiga marufuku maandamano ya upinzani katika miji mikuba

    Serikali nchini Kenya imepiga marufuku maandamano katika maeneo ya katikati mwa miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

    Kaimu waziri wa usalama Dkt Fred Matiang'i amesema pia kwamba wanaopanga maandamano wanafaa kuwajibishwa kutokana na uharibifu wa mali unaotokea wakati wa maandamano.

    Hatua ya Dkt Matiang'i imetokea huku muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) wake Raila Odinga ukiendelea na maandamano ya kushinikiza mageuzi katika Tume ya Uchaguzi (IEBC).

    Ijumaa hata hivyo polisi walikabiliana na waandamanaji ambao walijitokeza kwenye miji hiyo.

    Mmoja wa viongozi wa Nasa James Orengo, ambaye alikuwa naibu ajenti mkuu wa Bw Odinga wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti ambao ulifutiliwa mbali na Mahakama ya Juu, alitoa wito kwa wafuasi wa muungano huo kuandamana kila siku.

    Wakati huo huo tume hiyo ya Uchaguzi imetakiwa na mahakama kumjumuisha mgombea wa urais kwa chama cha thirdway Alliance kwenye uchaguzi mpya unaopangiwa Oktoba 26.

    Awali mgombea wa muungano wa upinzani NASA alijiondoa kwenye uwaniaji huo akisema bado maafisa wa IEBC waliotuhumiwa na mahakama kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Agosti 8 wangali ofisini.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako