• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Novemba-10 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-10 19:09:46
    Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa

    Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amemfuta kazi makamu wake Bw Emmerson Mnangagwa kwa kile alichodai ni utovu wa nidhamu.

    Akitangaza uamuzi wa Rais Mugabe, waziri wa habari wa nchi hiyo, Bw Simon Moyo, amesema katiba ya Zimbabwe inampa Rais madaraka ya kufanya hivyo. Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitano kwa Rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake, baada ya kufanya hivyo mwaka 2014 alipomfukuza Bibi Joyce Mujuru kwa madai ya kula njama za kumpindua.

    Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa kazi siku ya Jumatatu amelitoroka taifa hilo kufuatia vitisho vya kifo , kulingana na washirika wake.

    Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amemshtumu aliyekuwa makamu wake kwa kupanga njama za kuchukua mamlaka kutoka kwake.

    Naye Bi Mugabe amekuwa akipigania kung'atuliwa kwa makamu huyo katika mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi Ujao.

    Chama cha Zanu PF kilimfurusha Mnangagwa katika chama hicho siku ya Jumatano.

    Bwana Mugabe alimtaja naibu wake wa zamani kuwa miongoni mwa waliopanga njama na akaonya kuwa atawachukulia hatua maafisa wengine wa chama hicho walioshirikiana na Mnangagwa.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako