• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (6 Novemba-10 Novemba)

    (GMT+08:00) 2017-11-10 19:09:46

    Donald Trump wa Marekani afanya ziara yake ya kitaifa nchini China.

    Rais wa Marekani Donald Trump wiki hii amefanya ziara yake ya kitaifa nchini China

    Hii ni ziara ya kwanza kwa rais Trump nchini China tangu alipoapishwa kuwa rais wa Marekani, pia ni ziara ya kwanza ya kitaifa nchini China baada ya kufungwa kwa Mkutano mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China.

    Licha ya shughuli za kitaifa, Donald Trump amefanya mazungumzo na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing kufuatia makaribisho ya kkifahari.

    Wakati wa ziara hiyo, marais hao wawili waliajadili masuala muhimu yanayofuatiliwa na nchi zao, na kufikia maoni mapya ya pamoja, kuzidisha maelewano na urafiki, kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye sekta mbalimbali, ili kusonga mbele uhusiano kati ya China na Marekani katika zama mpya.

    Awali Trump alizuru Korea Kusini ambapo alikutana na rais Moon Jae-in na kusisitiza tena kanuni za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya amani na kuihimiza Korea Kaskazini kusimamisha mpango wa makombora ya nyuklia.

    Pande hizo mbili zimesema, kuendelea na silaha za nyuklia kwa Korea Kaskazini kutafanya nchi hiyo itengwe kidiplomasia na kuwa na hali ngumu kiuchumi.

    Kama nchi hiyo itaweza kutimiza hali isiyo na silaha za nyuklia kwa njia ya pande zote inayoweza kukaguliwa, na isiyoweza kurejesha hali ya zamani, peninsula ya Korea itapata amani ya kudumu.

    Habari nyingine zinasema, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesisitiza tena msimamo wa China kuhusu suala la nyuklia la Peninsuala ya Korea, akizitaka pande husika kufanya juhudi za pamoja kupunguza hali ya wasiwasi ya peninsula hiyo, na kurejesha suala hilo katika meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako