• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (March 17-March 23)

    (GMT+08:00) 2018-03-23 17:44:45

    Rais wa Myanmar ajiuzulu

    Rais wa Myanmar Hatin Kyaw amejiuzulu, wiki hii hayo ni kwa mujibu wa afisi yake.

    Hakuna sababu ilitolewa lakini kumekuwa na wasiwasi katika miezi ya hivi karibuni kuhusu afya ya rais huyo mwenye umri wa miaka 71 baada ya kuonekana amedhoofika katika hafla moja.

    Htin Kyaw alliapishwa kuwa rais 2016 baada ya uchaguzi uliositisha miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi.

    Lakini alikuwa kiongozi asiye na mamlaka huku aliyekuwa kiongozi wa upinzani wa muda mrefu Aung San Suu Kyi akiwa kiongozi mwenye mamlaka.

    Taarifa iliochapishwa katika mtandao wa facebook wa rais huyo ilisema kuwa Hatin alitaka kupumzika.

    Makamu wa rais Myint Swe , jenerali wa zamani atakuwa kaimu rais hadi pale rais mpya atakapochaguliwa katika muda wa siku saba sijazo, taarifa hiyo ilisema.

    Bi Suu Kyi, ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa chini ya uongozi wa kijeshi wa Junta alipigwa marufuku kuchukua wadhfa huo.

    Kipengee cha katiba kilichotengezwa ili kuhakikisha achukui wadhfa huo kinasema kuwa hakuna raia mwenye watoto kutoka nje anaweza kuwa rais.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako