• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 2-Juni 8)

  (GMT+08:00) 2018-06-08 20:39:54

  Mabaki ya ndege ya kampuni ya FlySax iliyopotea yapatikana katika eneo la Aberdares

  Maringa alisema mabaki hayo ya ndege ya 208 Cesna yenye nambari ya usajili wa 5Y-CAC yalipatikana mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri siku ya alhamisi kufuatia operesheni kali ya usakaji wa ardhini uliotekelezwa na wataalam wa jeshi. Kundi la waokoaji wakiwemo madaktari watakaoshirikiana na maafisa wa msalaba mwekundu tayari limepelekwa katika eneo hilo. Ndege hiyo ilitoweka kwa saa 36 na juhudi za kuitafuta siku ya Jumatano ziliathiriwa na hali mbaya ya anga.Ndege hiyo inayodaoiwa kufanyiwa ukaguzi wa mitambo mara kwa mara ilikuwa imesafiri kuelekea Homabay na Maasai Mara mapema siku ya Jumanne kabla ya safari hiyo ya kuelekea Nairobi.

  Marubani wake wawili waliripotiwa kuwa na uzoefu na inahofiwa kwamba ilipaa na kuingia katika eneo lenye hali mbaya ya anga juu ya mlima wa Aberdare katika eneo la Kinangop huko Nyandarua ambapo mawimbi yake ya simu yalipatikana mwendo wa saa kumi na moja jioni siku ya Jumatano.

  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako