• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 2-Juni 8)

  (GMT+08:00) 2018-06-08 20:39:54

  Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza atangaza kwamba hataomba kuchaguliwa tena baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2020

  Alitoa tangazo hilo akiwa eneo la Bugendana, Gitega ambapo alikuwa anaidhinisha katiba mpya ya nchi hiyo.

  Mwezi uliopita, raia nchini humo walipiga kura na kuunga mkono kwa wingi marekebisho ya katiba ambayo yalifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo kubadilisha muhula wa rais kutoka miaka mitano kuwa saba.

  Kwa sasa wengi wanatarajiwa kutakuwa na mabadiliko katika baraza la mawaziri karibuni.Aliwania kwa muhula wa tatu mwaka 2015 hatua iliyozua utata na kusababisha msururu wa ghasia na jaribio la mapinduzi ya serikali.

  Mamia ya watu walifariki na wengine 400,000 kukimbia nchi hiyo na kutorokea mataifa jirani.

  Burundi imebadilisha katiba yake mara kadhaa miaka ya hivi punde.

  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako