• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 9-Juni 15)

    (GMT+08:00) 2018-06-15 19:00:04

    Bemba aondoka ICC

    Aliyekua makamu wa rais nchini DRC, Jean Pierre Bemba, ameondoka kituo cha Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) alipokua akizuiliwa huko Hague nchini Uholanzi, siku moja tu baada ya majaji kuagiza kuachiliwa huru kwa masharti.

    Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC wameagiza kuachiwa huru kwa masharti kwa aliyekuwa makamu wa rais wa zamani wa DRC, Jean-Pierre Bemba ambaye juma lililopita alifutiwa mashtaka ya makosa ya kivita na dhulma dhidi ya binadamu.

    Bemba mwanasiasa maarufu nchini mwake na mpinzani mkubwa wa rais Joseph Kabila ameachiwa baada ya kushinda rufaa aliyokata kwenye mahakama hiyo kupinga adhabu ya kifungo cha miaka 18 jela baada ya kukamatwa nchini Ubelgiji mwaka 2016.

    Bemba alipatikana na hatia mwezi Machi mwaka 2016 kwa makosa ya uhalifu, uliotokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003 na akahukumiwa 21 Juni.

    Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo kufuatia rufaa aliyoiwasilisha kupinga hukumu hiyo.

    Hata hivyo majaji wa mahakama hiyo wamemuachia kwa masharti ya kutozungumza na vyombo vya habari wala kuwasiliana na mashahidi katika kesi yake, akisubiri hukumu kuhusu tuhuma za kuhonga mashahidi na kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.

    Ikiwa Bemba ataachiwa huru anatajwa kuwa kinara katika siasa za nchi hiyo na tayari chama chake cha MLC kinamtaja kama mgombea wao katika uchaguzi wa Desemba 23 mwaka huu.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako