• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 15-Septemba 21)

  (GMT+08:00) 2018-09-21 20:30:59

  Korea Kaskazini na Korea Kusini zasaini makubaliano ya Pyongyang

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini wiki hii wamesaini makubaliano ya Pyongyang yanayolenga kuondoa tishio la silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea.

  Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Korea Kaskazini imeahidi kufunga kiwanja kilichokuwa kikitumika kwa majaribio ya silaha za nyuklia.

  Pia kama Marekani itaendelea kufuata azimio la pamoja na Korea Kaskazini, Korea Kaskaizini itasimamisha kabisa mpango wake wa nyuklia.

  Pia Korea Kusini na Korea Kaskazini zimeamua kuondoa tahadhari ya kijeshi kati yao ili kuondoa tishio la vita katika peninsula hiyo.

  Habari zinasema, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un atatembelea Seoul, Korea Ksuini, katika siku za karibuni.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako