• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 15-Septemba 21)

  (GMT+08:00) 2018-09-21 20:30:59

  Russia na Uturuki kuanzisha eneo lisilo la kijeshi kwenye mkoa wa Idlib nchini Syria

  Rais Vladimir Putin wa Russia wiki hii amekutana na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye alifanya ziara nchini Russia.

  Baada ya mkutano wao marais hao wawili walitoa taarifa ya pamoja wakitangaza kuanzisha eneo lisilo la kijeshi kati ya jeshi la serikali na jeshi la upinzani kwenye mkoa wa Idlib nchini Syria.

  Taarifa imesema eneo hilo litasimamiwa na kikosi cha doria kitakachoundwa na wanajeshi wa Uturuki na polisi wa Russia. Pande hizo mbili pia zimependekeza kurudisha mawasiliano ya barabara kutoka mkoa wa Aleppo hadi Lattkia, na kutoka Aleppo hadi Hamah.

  Pande hizo zimesisitiza kuwa zitapambana na ugaidi wa aina mbalimbali nchini Syria, na kuchukua hatua kuhimiza utatuzi wa suala la Syria, chini ya mfumo wa mazungumzo ya amani ya Geneva, ili kutimiza amani ya Syria mapema.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako