• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 22-Septemba 29)

    (GMT+08:00) 2018-09-28 19:10:36

    Kipindpindu chaua zaidi ya watu 67 Niger

    Mlipuko wa Kipindpindu umeua watu zaidi ya 67 nchini Niger, miongoni mwa wagonjwa kadhaa walioorodheshwa, hasa katikaJimbo la Maradi, karibu na Nigeria, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ukinukuu ripoti kutoka Wizara ya Afya ya Niger.

    Ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa ya tarehe 10 Septemba mwaka huu ilibani kwamba watu 55 kwa jumla ya 2,752 walifariki dunia". Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jimbo la Maradi, katikati-kusini mwa Niger, karibu na Nigeria, limekuwa ni chanzo cha ugonjwa huo, kwa vifo 55 na kesi 3,232 zilizotambuliwa.

    Lakini hadi sasa, wagonjwa wachache bado wamehifadhiwa katika maeneo yaliyotengwa ili kuwahudumia kumatibatbu wagonjwa bila malipo.

    Wizara ya Afya imeonya kwamba janga hilo limesambaa, kwa mikoa mitatu, ikiwa ni pamoja na Dosso (kusini magharibi), Tahoua (magharibi) na Zinder (kusini-kati).


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako