• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 20-Oktoba 26)

    (GMT+08:00) 2018-10-26 19:27:30

    Zanzibar yakumbwa na uhaba wa mafuta

    Serikali ya Zanzibar imesema Zanzibar inakumbwa na uhaba wa mafuta, unaosababisha msongamano kwenye vituo vya mafuta.

    Mkuu wa Mamlaka ya usimamizi wa huduma za nishati na maji wa Zanzibar Bw. Haji Kali, amethibitisha kuwepo kwa hali hiyo, akisema Zanzibar imebaki na akiba ya lita laki 5.2 za mafuta, zinazoweza kukidhi mahitaji ya siku tatu tu.

    Ameongeza kuwa serikali inajitahidi kuagiza mafuta kutoka nje ili kutatua hali hiyo.

    Amewataka madereva na wananchi wawe watulivu.

    Amesema zaidi ya tani 880 za mafuta yaliyoagizwa wiki iliyopita, hayaruhusiwi kuingia kwenye soko kutokana na tatizo la ubora, ambalo kiasi cha maji kwenye mafuta hayo kimefikia asilimia 2.5, ambacho ni zaidi ya kigezo cha asilimia 0.02.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako