• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 20-Oktoba 26)

    (GMT+08:00) 2018-10-26 19:27:30

    Theresa May asema Uingereza na Umoja wa Ulaya wamekubaliana kwa asilimia 95 juu ya makubaliano ya Brexit

    Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesema Uingereza na Umoja wa Ulaya wamefikia mwafaka kwa asilimia 95 juu ya makubaliano ya uhusiano wa pande mbili baada ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Akiwahutubia wabunge kwenye baraza la makabwela, Bibi May amesema Uingereza ina uhuru wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya wakati wowote, na haitaki mpango wowote unaozuia uhuru huo, na kwamba suala kubwa ambalo bado halijatatuliwa ni hatma ya mpaka kati ya Ireland Kaskazini na Jamhuri ya Ireland.

    Bibi May amesisitiza kuwa matokeo mazuri zaidi kwa Uingereza, Ireland na Umoja wa Ulaya ni kwamba uhusiano wa baadaye utakubaliwa na kutekelezwa kabla ya Januari mosi mwaka 2021.

    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako