• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 5-January 11)

  (GMT+08:00) 2019-01-11 18:56:22

  Jimbo linalojiendesha la Puntland nchini Somalia lachagua rais mpya

  Waziri wa zamani wa mpango wa Somalia Bw. Sa'id Abdulahi Deni amechaguliwa wiki hii kuwa rais wa jimbo linalojiendesha la Puntland kwa muhula wa miaka mitano.

  Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na baraza la chini la bunge la Puntland Bw. Abdihakim Mohamed Ahmed (Dhobo) ametangaza matokeo hayo, ambapo Bw. Deni alipata kura 35 na mgombea wake Bw. Asad Osman Abdulahi alipata kura 31 kwenye duru ya tatu ya upigaji kura.

  Rais huyo mteule amewashukuru wajumbe wa baraza la chini la bunge la Puntland kwa kumpigia kura na kumwunga mkono kuongoza jimbo hilo katika miaka mitano ijayo.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako