• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 5-January 11)

  (GMT+08:00) 2019-01-11 18:56:22

  Waziri mkuu wa Uingereza asisitiza makubaliano ya Brexit yapigiwe kura wiki ijayo kama ilivyopangwa

  Waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amesisitiza kuwa upigaji kura wa makubaliano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya Brexit utafanyika kwenye Baraza la makabwela wiki ijayo kama ilivyopangwa.

  Bibi May amesema anatarajia kuwa makubaliano ya Brexit yatapitishwa, na kama yakishindwa kupitishwa, hatma ya Uingereza itaangukia kwenye hali ya sintofahamu.

  Wabunge wa upinzani na wanasiasa kutoka chama chake cha wahafidhina wametishia kupinga makubaliano ya Brexit. Kama wakifanya hivyo, kuna uwekezano mkubwa zaidi kwa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya bila makubaliano yoyote.

  Bibi May amesema Umoja wa Ulaya umekubali baadhi ya mabadiliko, na anaendelea kuzungumza na viongozi wa Ulaya, wakati anajaribu kuwapa wabunge imani ya kuyaunga mkono makubaliano aliyoyafikia na Umoja wa Ulaya.


  1  2  3  4  5  6  7  8  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako