• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Januari 12-January 19)

  (GMT+08:00) 2019-01-18 16:35:08
  Zaidi ya watu 20 wauwawa kwenye shambulizi la kigaidi Kenya

  Zaidi ya watu 20 wameuwawa wiki hii kwenye shambulizi la kigaidi lililotokea kwenye hotelimoja ya kifaharai mjini Nairobi nchini Kenya, kulingana na polisi.

  Inaaminika kuwa wapiganaji wa kundi la al-shabaab walitekeleza shambulizi hilo la Jumanne dhidi ya hoteli ya Dusit.

  Kamera za usalama zinaonyesha watu wane waliojihami wakiingia kwenye hoteli hiyo na kuanza kufyatua risasi huku mmoja wa wahambuliaji akijilipua.

  Polisi walifika haraka kwenye eneo hilo na kufanikiwa kuwaokoa zaidi ya watu 700 waliokuwa maeneo yote ya karibu na hoteli, kwenye opsaresheni ya usiku kucha.

  Saa 24 baada ya kumalizika kwa shambulio hilo, polisi wameendesha msako mkali na kuwakamatza zaidi ya watu 20 wanaohusishwa na upangaji wa shambulizi hilo.

  Shirika la msalaba mwekundu la Kenya KRCS limesema watu 94 walioripotiwa kutojulikana walipo baada ya kutokea kwa shambulizi wamepatikana.

  Shirika hilo limesema watu hao 94 wote walipatikana, na sasa limeanza kuwapa ushauri nasaha walionusurika na familia za wahanga 21 waliouawa katika shambulizi hilo.

  Hatua hiyo imekuja baada ya polisi nchini Kenya kutangaza kuwa shambulizi hilo lililotokea kwenye eneo la Riverside Drive limesababisha vifo vya watu 21 na wengine wengi kujeruhiwa.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako