• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 22-Juni 28)

  (GMT+08:00) 2019-06-28 18:23:19

  Mkuu wa jeshi wa Ethiopia auwawa

  Kiongozi wa Jeshi la nchi Ethiopia, Jenerali Seare Monnen, ameuawa wiki hii kwa kupigwa risasi na mlinzi wake mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

  Yeye na ofisa mwingine walipoteza maisha katika mji wa Amhara wakijaribu kuzuia mapinduzi dhidi ya utawala nchini humo.

  Mjini Ahmara kwenyewe, gavana wa mji huo Ambachew Mekonnen aliuawa pamoja na mshauri wake.

  Bendera zinapepea nusu mlingoti baada ya serikali kutangaza kuwa siku ya maombolezo.

  Jenerali Saare na Gavana wa Amhara, bwana Ambachew Mekonnen walikuwa wakionekana kama washirika wakubwa wa Waziri Mkuu Abiy.

  Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yameikumba Amhara na miji mingine miaka ya hivi karibuni.

  Waziri mkuu alikwenda kwenye kituo cha Televisheni akiwa na mavazi ya kijeshi kukemea mashambulizi hayo.

  Tangu uchaguzi wa mwaka jana, Abiy amekua akipambana kumaliza mvutano wa kisiasa kwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kuondoa makatazo dhidi ya vyama vya kisiasa na kuwashtaki maafisa wanaoshutumiwa kukiuka haki za binaadamu.

  Kiongozi wa jeshi anayeshukiwa kuongoza jaribio la mapinduzi siku ya Jumamosi katika eneo la Amhara, ameuawa na polisi.


  1  2  3  4  5  6  7  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako