• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 22-Juni 28)

    (GMT+08:00) 2019-06-28 18:23:19

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa laongeza vikwazo dhidi ya DRC

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu kuongeza muda wa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC hadi Julai 1, 2020.

    Azimio hilo No. 2478 limeungwa mkono na wajumbe 15 wa Baraza hilo, ambalo pia limeongeza muda wa idhini ya Kundi la Wataalamu wanaosaidia kamati ya vikwazo hadi Agosti 1, 2020.

    Azimio hilo linalitaka kundi hilo kuwasilisha ripoti ya kipindi cha kati kwenye Baraza la Usalama kabla ya Desemba 30, 2019, kutoa ripoti ya mwisho kabla ya Juni 15, 2020, pamoja na taarifa ya mwezi kwenye Kamati ya vikwazo.

    Umoja wa mataifa aidha unaitaka Serikali ya DRC kuharakisha uchunguzi wa mauaji ya wataalamu wake wawili pamoja na raia wanne wa nchi hiyo waliouawa mwezi Machi mwaka 2017.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako