• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (July 13-July 19)

    (GMT+08:00) 2019-07-19 21:32:46

    Jaguar azuru Tanzania

    Siku chache tu baada ya kutoa matamshi yaliozua utata nchini Tanzania, mbunge wa Starehe nchini Kenya Charles Kanyi Jaguar yupo nchini Tanzania .

    Kiongozi huyo ambaye picha zake za mtandao wa Instagram zimemuonyesha akiwa mjini Dar es Salaam na Dodoma nchini Tanzania amesisitiza taarifa yake ya awali akisema kwamba aliyeleweka vibaya kuhusu matamshi aliyotoa kuhusu raia wa kigeni wanaoishi nchini Kenya. Kiongozi huyo ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya amesema kwamba yuko nchini Tanzania kwa siku nne kuijulia hali familia yake mbali na kuwatembelea marafiki zake. Msanii huyo wa wimbo wa 'Kigeugeu' amesema kwamba anapanga kukutana na wabunge marafiki zake wa taifa hilo kama vile Profesa J na Sugu pamoja na wasanii tofauti.

    Kiongozi huyo alizua utata nchini Tanzania aliponukuliwa katika kanda moja ya video iliosambaa katika mitandao ya kijamii akiwataka raia wa kigeni wanofanya biashara nchi humo kufurushwa.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako