• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 17-August 23)

    (GMT+08:00) 2019-08-23 19:44:00

    Waziri mkuu mpya wa Sudan aapishwa

    Viongozi wa kijeshi na wale wa muungano wa upinzani wametangaza kuundwa kwa baraza huru la uongozi ambalo litatawala kwa mpito katika kipindi cha miaka 3 kuelekea kupata serikali ya kiraia.

    Baraza hilo lenye wajumbe 11, limetangazwa na msemaji wa baraza la mpito la kijeshi ambalo limekuwa likitawala tangu kuangushwa kwa utawala wa Omar al-Bashir mwezi April mwaka huu.

    Sasa Waziri mkuu mpya wa Sudan ni Bw. Abdalla Hamdok na amesema, jukumu la kwanza la serikali yake ni kutimiza amani na kujenga uchumi imara.

    Bw. Hamdok baada ya kuapishwa amesema, serikali yake itafanya juhudi kusimamisha vita, kutimiza amani ya kudumu na kujenga uchumi imara wa taifa kwenye msingi wa uzalishaji.

    Ameongeza kuwa, serikali mpya itafanya mageuzi kwa taasisi za serikali, kupambana na ufisadi na kujenga utawala wa sheria, usawa na haki.

    Awali wiki hii Abdel Fattah al-Burhan aliapishwa rasmi mbele ya baraza la kisheria kuwa mwenyekiti wa baraza jipya la pamoja la utawala la Sudan.

    Al-Burhan amekula kiapo kikatiba mbele ya Kaimu Jaji mkuu Yahia al-Tayeb Abu Shoura katika ikulu ya rais mjini Khartoom. Al-Burhan aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan TMC alitangaza amri ya katiba ya kuunda baraza jipya la utawala lenye wajumbe 11.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako