• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (August 17-August 23)

    (GMT+08:00) 2019-08-23 19:44:00

    Maduro asema yupo kwenye mazungumzo na utawala wa Donald Trump

    Rais wa wa Venezuela Nicolás Maduro amesema yupo kwenye mazungumzo na utawala wa raisi Donald Trump kwa miezi kadhaa sasa - licha ya vikwazo vipya vya Marekani kwa taifa hilo.

    Mgogoro unaoedelea wa kisiasa na kiuchumi umeianya Venezuela kuwa na marais wawili waliojitangazia uhalali wa kuongoza.

    Marekani ni moja ya mataifa 50 ambayo hayamtambui Maduro kama raisi halali wa Venezuela.

    Utawala wa Washington ulitangaza vikwazo vipya dhidi ya Venezuela mwanzoni mwa mwezi kama njia ya kumuongezea Maduro shinikizo la kung'atuka.

    Hata hivyo Jumanne, Maduro amethibitisha kuwa amekuwa kwenye mazungumzo na maafisa waandamizi wa serikali ya Trump kwa miezi kadhaa sasa.

    Akizungumza kupitia runinga, Maduro amesema: "Kama nilivyofanya mazungumzo ndani ya Venezuela, pia nimetafuta namna ya kumfanya raisi Trump aisikilize Venezuela."

    Raisi Trump pia amethibitisha kuwa utawala wake umekuwa kwenye "mazungumzo na wawakilishi wa Venezuela".

    Taifa hilo limekabiliwa na mgogoro wa uongozi kati ya rais Maduro na kiongozi wa bunge la Venezuela , Juan Guaidó.

    Bwana Guaidó alijitangaza mwenyewe kuwa kaimu rais mnamo mwezi Januari , akidai kwamba uchaguzi uliomleta maduri uongozini kwa muhula wa pili ulikumbwa na udanganyifu.

    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako