• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 12-Oktoba 18)

    (GMT+08:00) 2019-10-18 19:20:18

    Syria yaziba njia muhimu iliyokusudiwa kutumiwa na Uturuki, kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani kwazua mjadala.

    Vikosi vya serikali ya Syria vimeingia katika mji wa kimkakati wa Kobani, kuziba njia moja ambayo Uturuki iliazimia kuitumia, wakati hatua ya Trump kuondoa wanajeshi Syria ikileta mgongano Marekani. Vikosi vitiifu kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad vimeingia katika mji wa Kobani usiku wa kuamkia leo, hatua inayobadilisha hali ya mambo Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Mjini Kobani ndipo jeshi la Marekani lilipounda ushirika na wapiganaji wa Kikurdi katika vita dhidi ya Kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

    Kudhibiti mji huo kunaipa serikali ya rais Assad kuzuia mipango ya Uturuki kuunganisha maeneo madogo yaliyo chini ya uangalizi wake kaskazini magharibi mwa Syria, na mengine maogo iliyoyakamata kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wiki iliyopita, ili kuunda ukanda salama wenye upana wa km 30, kati ya mpaka wake na wapiganaji wa Kikurdi inaowachukulia kuwa magaidi. Huku hayo yakijiri, Marekani yazidi kuihama miji ya Syria.

    Siku ya Jumatano Jeshi la Marekani lilitangaza kukihama kiwanda cha saruji kusini mwa Kobani, ambacho ilikitumia kama kituo cha uratibu wa ushirikiano wake na wapiganaji wa kikurdi. Marekani pia iliipa kisogo miji mingine muhimu ya Raqqa na Tabqa, na msemaji wa ushirika wa kijeshi ilioongoza dhidi ya IS Kanali Myles Caggins, alisema kuwa wameziharibu shehena za silaha walizoziacha nyuma kwa kutumia ndege za kivita.

    Mmoja wa makamanda wa jeshi la Syria Ahmad Hussein ameseme kuingia katika eneo hilo ni hatua muhimu kijeshi.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako