• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 12-Oktoba 18)

    (GMT+08:00) 2019-10-18 19:20:18

    AS Roma imekuwa timu ya kwanza Ulaya kufungua akaunti ya Twitter kwa lugha ya Kiswahili.

    Klabu ya mpira ya 'As Roma' nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza kutoka barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter. Kurasa hiyo ya As Roma itakuwa ikiandika habari zake kwa lugha adhimu ya kiswahili.

    Ukurasa huo wa lugha ya kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanatumia lugha ya kiswahili. Akaunti hiyo ya Twitter imezinduliwa siku ya jumatano kwa video yenye maneno ya utani ya kiswahili.

    Akaunti hiyo imepokelewa vizuri na wasomaji wa kiswahili wa Tanzania na Kenya. Wengi wakiona kuwa ni ubunifu mzuri ambao unaonesha kuwajali mashabiki wanaoongea lugha ya Kiswahili. Idadi kubwa ya watu wameanza kufuatilia kurasa hiyo na kujibu kwa kiswahili. Rais wa klabu hiyo Jim Pallotta ametumia kurasa yake binafsi ya tweeter kuthibitisha kuwa kurasa hiyo imefunguliwa. Uzinduzi huu umekuja baada ya maombi ya mashabiki kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika ya kati na mataifa mengine ya mashariki na kusini mwa Afrika.

    Mapenzi ya soka la ulaya kutoka ukanda huu wa Afrika unastaajabisha kwa nini klabu za mpira za nje ya bara hilo kushindwa kuwasiliana kwa lugha ya kiswahili au Pidgin kabla ya mitandao ya kijamii. Kuna kurasa nyingine rasmi za lugha ya kiitaliano, kiingereza, kiarabu,kifaransa, kireno, kichina, lugha ya Uturuki, Bosnian, , Dutch, Farsi na Pidgin.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako