• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 19-Oktoba 25)

  (GMT+08:00) 2019-10-25 20:59:57
  Mwanariadha Eliud Kipchoge atunukiwa tuzo ya juu ya Rais

  Mwanariadha wa Kenya bingwa wa Olimpiki katika mashindano ya marathon, Eliud Kipchoge ametunukiwa tuzo ya kitaifa na rais Uhuru Kenyatta.

  Rais Kenyata ambaye aliongoza sherehe za Sikukuu ya Mashujaa mjini Mombasa,pwani ya Kenya,jumapili iliyopita,amemsifu mwanariadha huyo kwa kuwa mtu wa kwanza kuwahi kukimbia kilomita 42 chini ya saa mbili mjini Vienna.

  Wakati wa maadhimisho ya sherehe za siku ya Mashujaa,Rais Kenyatta alimpa tuzo ya Elder of the Golden Heart (EGH) mwanariadha mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge,kwa kuwa mtu wa kwanza duniani kukimbia mbio za kilomita 42 chini ya masaa mawili.

  Rais alisema Kipchoge aliuhakikishia ulimwengu kuwa hakuna juhudi zozote za binadamu ambazo zinaambulia patupu,na kwamba kila lengo linaweza kufikiwa.


  1  2  3  4  5  
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako