• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 19-Oktoba 25)

    (GMT+08:00) 2019-10-25 20:59:57

    Mahakama ya juu Tanzania yabatilisha sheria ya ndoa za utotoni

    Mahakama ya juu zaidi Tanzania imebatilisha sheria inayoruhusu familia kuwaoza wasichana wadogo wenye umri wa kuanzia miaka 14.

    Mahakama kuu ya rufaa imebatilisha uamuzi uliotolewa awali na mahakama nyingine nchini kwa misingi ya kuwa ndoa za watoto zinakiuka haki za wasichana, na nii kinyume cha sheria na katiba ya nchi hiyo.

    Mwanasheria mkuu wa Tanzania alikuwa amekata rufaa juu ya uamuzi wa mahakama ya juu wa mwaka 2017, ambapo ilikuwa imeondoa vipengele vya sheria na kuruhusu ndoa kwa wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 14.

    Mahakama alhamisi ilisema kuwa wasichana hawawezi kuolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, umri ambao wavulana pia wanaruhusiwa kuoa.

    Uamuzi huu wa mahakama ni hatua iliyopigwa katika kutetea haki za wasichana. Taarifa ya kuzuiwa ndoa za mapema kwa wasichana imepokelewa kwa hisia mbali mbali katika mitandao ya kijamii.

    Shirika la Msichana Initiative ambalo ndilo lililowasilisha kesi mahakamani kupinga sheria ya kuolewa kwa wasichana wadogo, limesema: "Maamuzi ya leo ni maamuzi muhimu kwa wasichana wa leo na wa baadae.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako