• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 9-Novemba 15)

    (GMT+08:00) 2019-11-15 20:19:23

    Jimbo la Kano,Nigeria laanzisha malipo ya kodi ya harusi

    Ni takribani miezi minne sasa hakuna ndoa iliyofungwa katika kijiji kimoja la jimbo la Kano, nchini Nigeria tangu chifu wa eneo hilo kuanzisha malipo ya kodi ya harusi.

    Ado Sa'id, ambaye ni chifu wa kijiji cha Kera kaskazini magharbi mwa Nigeria, amewataka mabwana harusi kulipa kodi ya kiasi cha dola 377.

    Hii ikiwa ni mbadala wa utamaduni ambao uliopo wa kulipa samani, vyombo vya jikoni na vitu vingine vya thamani kwa ajili ya kutoa kwa familia ya bibi harusi watakapofunga ndoa.

    Kiongozi huyu amesema kuwa kulipa kodi ni rahisi zaidi kuliko kulipa mahari na itawafanya watu wengi kufunga ndoa kirahisi.

    Alisema utekelezaji utaanza baada ya kushauriana na wanakijij, jambo amalo lilipingwa vikali.

    Wanakijiji wanahisi kuwa utaratibu uliokuepo zamani ulikuwa mzuri na walikuwa wanaweza kununua zawadi wanavyotaka.

    Mwanakijiji mmoja , Isah Kera, anasema kuwa sheria mpya inawalazimisha wapenzi kwenda kufunga ndoa sehemu nyingine ili kukwepa kodi hiyo.

    Mwanakijiji mwingine, Sani Kera anasema kuwa ana watoto watano ambao wako tayari kuoa ,lakini mipango yao imebidi ihairishwe.

    Wakati Nigeria wanalalamikia kodi kwenye harusi, vijana wa mataifa ya Afrika mashariki wamekuwa wanalalamikia gharama ya mahari inayotolewa katika jamii mbalimbali.


    1  2  3  4  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako