• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 23-Novemba 29)

    (GMT+08:00) 2019-11-29 19:17:46

    Watu 36 wafariki kutokana na mvua kunywa DRC

    Watu wasiopungua 36 wamefariki dunia baada ya mvua kubwa kunyesha Jumatatu usiku wiki hii katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa. Naibu Gavana wa mji huo, Neron Mbungu amesema. Naibu Gavana wa mji huo, Neron Mbungu amesema shughuli ya kutafuta miili mingine ya watu waliofariki dunia au manusura linaendelea. Mvua hiyo imesababisha uharibifu wa vifaa na hasara kwa binadamu. Waathiriwa walipelekwa na maporomoko ya udongo. Madaraja mawili yameporomoka na barabara inayoelekea chuo kikuu katika Wilaya ya Lemba, imeharibika vibaya. Mwaka wa 2018 mamia ya watu walfariki dunia kutokana na mmomonyoko na maporomoko katika mji wa Kinshasa baada ya mvua kubwa kunyesha usiku kucha. Kinshasa ni mji wa tatu wenye watu wengi barani Afrika, una wakaazi milioni 10, ambao wengi wao wanaishi katika nyumba ambazo ni rahisi kuporomoka mvua inaponyesha.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako