• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 23-Novemba 29)

    (GMT+08:00) 2019-11-29 19:17:46
     

    Karibu watu 20 wauawa na waasi DRC

    Karibu watu 20 wanadaiwa kuuawa katikia eneo la Beni na waasi Uganda ADF. Siku ya jumatano, miili kumi na tisa ilipatikana katika eneo la Maleki, karibu kilomita kumi kutoka mji wa Oicha, katika Wilaya ya Beni, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa.

    Wahanga waliuawa kwa mapanga na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la waasi wa Uganda wa ADF. Mauaji haya yanatokea mbili baada ya maandamano makubwa dhidi ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, maandamano yaliyokumbwa na vurugu na kusababisha vifo wilayani Beni.

    Shambulio hilo lilitokea kama kilomita 10 kutoka kambi ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa. Ripoti ya kwanza iliyotolewa na asasi za kiraia ilibaini kwamba watu 14 waliuawa saa kumi na mbili asubuhi. Sasa idadi hiyo imeongezeka hadi 19.

    Wilaya ya Beni imeendelea kukumbwa na zimwi la mauaji, huku raia wakiendelea kulalamikia usalama wao.


    1  2  3  4  5  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako