• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Desemba 7-Desemba 13)

    (GMT+08:00) 2019-12-13 20:26:14

    Waziri Mkuu wa Ethiopia ashinda tuzo ya amani ya Nobel

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mjini Oslo akitoa wito wa kuwepo umoja huku machafuko ya kikabila yakiitikisa nchi yake na juhudi za suluhu pamoja na Eritrea zikionyesha kukwama.

    Abiy Ahmed mwenye umri wa miaka 43 ameshinda tuzo ya amani ya Nobel kwaajili ya juhudi zake za kuupatia ufumbuzi mzozo wa muda mrefu kati ya Ethiopia na Eritrea.Tuzo hiyo ni jaza pia kwa juhudi zake za upatanishi katika Afrika mashariki na mageuzi ya kidemokrasi aliyoyaanzisha nchini mwake, nchi iliyokuwa ikitawaliwa na waimla kwa muda mrefu.

    Akikabidhiwa tuzo hiyo Abiy amesifu mchango wa kiongozi wa Eritrea aliyemtaja kuwa "mshirika na ndugu katika juhudi za amani. Akimkabidhi tuzo hiyo mwenyekiti wa kamati ya amani ya Nobel Berit Reiss-Andersson amekumbusha shauku iliyokuwa awali imeanza kutoweka na waziri mshindi huyo wa tuzo ya amani anakabiliwa na changamoto kubwa. Mpaka kati ya nchi hizo mbili umefungwa na suala la mpaka bado mpaka sasa halijapatiwa jibu. Sherehe za kutunukiwa tuzo ya amani ya Nobel zimeingia dowa kwa kukataa waziri mkuu Abiy Ahmed kujibu masuala ya vyombo vya habari.

    Tuzo ya amani ya Nobel ni mchanganyiko wa medali ya dhahabu na kitita cha Kron milioni tisa za Sweeden ambazo ni sawa na Euro 850.000.


    1  2  3  4  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako