• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Aprili 4-Aprilii 10)

    (GMT+08:00) 2020-04-10 19:34:08

    Kenya USAMBAZAJI wa chakula dawa na maji, bila malipo, kwa wakazi masikini na wenye mahitaji maalum

    USAMBAZAJI wa chakula dawa na maji, bila malipo, kwa wakazi masikini na wenye mahitaji maalum ni baadhi ya hatua ambazo Gavana Ali Hassan Joho atachukua kukabiliana na makali ya marufuku iliyoanza kutekelezwa Jumatano.

    Gavana amesema serikali yake imetenga kitita cha Sh200 milioni kufadhili mpango huo.

    Aliongeza kuwa wafanyabiashara mabwanyenye kutoka kaunti hiyo pia wameahidi kutoa Sh100 miliioni kupiga jeki mpango huo ambao utaanza kutekelezwa.

    Kando na hayo mkuu huyo wa kaunti ya Mombasa amesema kaunti yake inaendelea kutumia Sh324 milioni kununua dawa na vifaa vya matibabu kwa hospitali za umma ili kuwasaidia wananchin wakati huu mgumu.

    amesema serikali yake itasaidia zaidi ya familia 200,000 zenye mahitaji maalum na kuwasambazia misaada ya chakula, dawa na maji chini ya mpango huo.

    Bw Joho alitoa hakikisho hilo saa chache baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza amri ya kuzuia watu kuingia na kutoka kaunti za Nairobi, Kilifi, Kwale na Mombasa ambazo zimeorodheshwa kama zile ambazo zimeathirika zaidi ya janga corona.

    Amri hiyo ilianza kutekelezwa Nairobi kuanzia Jumatatu saa moja za usiku kwa siku 21. Na kuaanza kutekelezwa Jumatano katika kaunti za Mombasa, Kilifi na Kwale kwa muda huo huo.


    1  2  3  4  5  6  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako